January 2, 2021


 KIPA wa Simba, Aishi Manula amefunguka kuwa kikosi chao kina nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, FC Platinum ya Zimbabwe na kufuzu hatua ya makundi.

 

Simba inatarajiwa kuwakaribisha Wazimbabwe hao katika mchezo wa marudiano unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza uliopigwa Zimbabwe kwa bao 1-0.


Simba inahitaji kupata ushindi wa kuanzia mabao 2-0 ili kuweza kufuzu hatua ya makundi ambayo hawakufanikiwa kufuzu msimu uliopita baada ya kuondolewa na UD Songo ya Msumbiji katika hatua za awali.


Kipa namba moja wa Simba Manula amesema tofauti ya bao 1-0 waliyonayo mpaka sasa haiwezi kuwa kikwazo kwao kufuzu.

 

"Kwanza niseme kila mmoja anajua kuwa tuko nyuma kwa bao 1-0 mpaka sasa, lakini ni wazi bado tuna nafasi kubwa ya kufuzu hatua ya makundi kwa kuhakikisha tunashinda mchezo wetu wa marudiano ambao tutacheza kwenye uwanja wa nyumbani hapa Dar es Salaam.

 

"Naamini matokeo mazuri kwenye michezo yetu miwili iliyopita yametuongezea morali ya kushinda mchezo huo, na kupitia sapoti ya mashabiki wetu na wadau wa soka hapa nchini tutafuzu na kwenda hatua ya makundi,” amesema Manula.

7 COMMENTS:

  1. Haitakiwi maneno inatakiwa vitendo haya msumbiji ilikiwa hivi tena wao walikiwa rahisi sana wepesi sana goli 1 tu lilitishinda mbwembwe nyingi tukatolewa hapo kwa mkapa sasa haitakiwi mbwebwe inataka vitendo

    ReplyDelete
  2. Nikiwa ni shabiki wa Yanga, basi nawaomba wana yanga wenzangu tuwe pamoja na timu ya nyumbani Simba kwasabsbu Mungu akipenda nasi kunyakuwa ubingwa nasi pia tutahitajia msaada wa Simba na ndivo ulivo uzalendo ili kulinyanyua jina la nchi yetu Tanzania

    ReplyDelete
  3. Nazani wewe ndio utakuwa mshabiki wa kwanza wa yanga na tza kutuombea duwa inshaalah tutashinda.

    ReplyDelete
  4. Nimependa maneno ya shabiki wa yanga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba mwisho wao kwa mkapa tarehe 5/01/2021 . Na ubingwa mpaka huu wasahau

      Delete
  5. Huu ni ulimwengu wa kistaarabu wacha chuki na hasada zako

    ReplyDelete
  6. wachezaji wa simba wanatakiwa kuonyesha ukubwa wao na ukubwa wa clab ya simba nawatakia kila la her

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic