January 3, 2021

 


IMEFAHAMIKA kuwa wachezaji wa Simba ndiyo waliomuondoa kikosini Jonas Mkude sambamba na kusimamishwa kazi kutokana na utovu wake wa nidhamu.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu uongozi wa timu hiyo kupitia kwa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez umsimamishe kiungo huyo ambaye wiki ijayo itamuita kwa ajili ya kutoa utetezi wake kwa utovu wa nidhamu ambao ameufanya.

 

Taarifa zimeeleza kuwa kabla ya uongozi kumpa barua ya kumsimamisha kazi, baadhi ya wachezaji waandamizi wa timu hiyo walimuwekea kikao na kumtaka abadili mwendo wake.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa wachezaji hao walichukua hatua hiyo baada ya kiungo huyo kuchelewa mara tatu mfululizo katika msafara wa mchezo wa Mbeya waliocheza dhidi ya Mbeya City, Nigeria walipokwenda kucheza na Plateau FC na ule wa Zimbabwe ambako walikwenda kukipiga na FC Platinum.

 

Aliongeza kuwa mara baada ya kikao hicho cha wachezaji kiungo huyo aliahidi kubadilika lakini alirudia kosa kwa kuondoka kambini huku simu yake akizima wakati timu hiyo ikijiandaa na mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Majimaji FC.

 

“Wachezaji ndiyo walikuwa wa kwanza kumuondoa kambini sambamba na kumtaka kocha wao Sven (Vandenbroeck) kutomchezesha michezo kumi mfululizo ya ligi na mashindano mengine.

 

“Hiyo ni baada ya kiungo huyo kushindwa kubadilika, licha ya kumuwekea kikao na kumtaka abadilike, hivyo wachezaji walikubaliana kwa pamoja kambini kwa kumuomba kutomtumia Mkude.

 

"Hivyo Mkude hautamuona katika michezo kumi hata kama uongozi ukimrudisha katika timu, pia kiungo huyo amechukuliwa posho za michezo kumi ambayo ameicheza ya ligi na mashindano ya kimataifa,” alisema mtoa taarifa.


Chanzo:Championi

9 COMMENTS:

  1. Angesimamishwa hadi ligi imalizike akatwe mshahara na posho asipewe aende akalewe anajiona yeye ndio bora sana kuliko simba afukunzwe aende huko kandambili

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mleten jangwan 2mpge bench muone Kama ataleta ngebe hizo

      Delete
  2. Hiyo sio dawa. watu kama hawa hawakosekani kabisa kwenye timu. kama wakina Gazza Leornado na wengine wengi. Kamati ya nidhamu impe last warning ndio kikubwa...... Mambo mengine mtu inabidi aombewe tu kila siku yeye shida nini unadhani......

    ReplyDelete
  3. Sasa wale waliokuwa wanavumisha kuwa kamtongoza ceo watasemaje, hadi ile redio fekiya efm

    ReplyDelete
  4. Tazama nidham ndani ya Simba. Wachezaji wenyewe ndio wanaoamuwa namna yakuhifadhi nidham kufikia hadi kukubaliana kwa pamoja kutoa adhabu anapotokea mkorofi katika timu yao iliyotulia. Kweli wana mahaba makubwa kwa timu pamoja na viongozi wao. Hawana chuki na mtu wala kulalamika ovyovyo na ndio siri kubwa ya maendeleo yao. Mungu Yarabi uzidi kuibariki Simba wala wasiwe na chuki kwa yoyote

    ReplyDelete
  5. Maoni ya mwandishi hii kaitoa jana kwenye gazeti lao leo kaileta huku huu wote ni uchochezi

    ReplyDelete
  6. sio uchochezi kama mchezaji hana nidham adhibiwe sio mara ya kwanza huyo mchezaji kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu au afukuzwe

    ReplyDelete
  7. Mambo haya hayana weledi kabisa.timu imemsimamisha mchezaji bila kubainisha kosa lake halis.nidhan ina mambo meng wangesema kwa uwaz kafanya kosa lipi? Linapoendela kufumbwa ndo maana waandishi wanapata mahali pa kufukuafukua kutnga story na kuiharibu timu na tasnia ya soka kwa ujumla

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bado haijulikan kosa lake viongoz wanakaa wiki hii kwa ajili ya hilo

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic