ITAFAHAMIKA baada ya dakika 90 nani atakuwa anacheka na nani atalia baada ya wanaume 22 kumaliza kazi yao ndani ya dakika hizo kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi.
Azam FC mabingwa mara tano wa Kombe la Mapinduzi baada ya kuondolewa na Yanga ambao ni mabinga wa kwanza wa Kombe la Mapinzudi ilikuwa msimu wa 2007 watashuhudia mpambano huu wakiwa kwenye makochi.
Vita yao leo itakuwa namna hii Uwanja wa Amaan:-
Wakuchungwa Kwa Simba
Miraj Athuman
Huyu ni mtambo wa mabao ndani ya Simba na Kombe la Mapinduzi kiujumla akiwa ametupia mabao manne kwenye mechi tatu ambazo amecheza.
Huyu anakazi ya kulindwa leo kwa kuwa ni mchezaji mwenye ushkaji na nyavu ana tuzo ya mchezaji bora aliipata kwenye mchezo dhidi ya Chipukizi.
David Kameta
Simba ikiwa imefunga jumla ya mabao 7, Kameta amewaga maji mara mbili,hivyo wapinzani wana kazi ya kumtazama mbeba mikoba ya Shomari Kapombe.
Francis Kahata
Amekuwa na mchango mkubwa ndani ya Kombe la Mapinduzi kwenye mechi zote tatu ambazo amecheza. Ana tuzo ya mchezaji bora aliipata kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC.
Meddie Kagere
Mshambuliaji ambaye amerejea kwenye ubora wake akiwa eneo la kufunga na mpira lazima akupe tabu. Kwenye Kombe la Mainduzi ametupia mabao mawili akipewa nafasi atao adhabu kwa mpinzani.
Kwa Yanga
Tuisila Kisinda
Spidi 120 kwenye miguu yake, mabeki wa Simba wana kazi ya kufanya kumzuia nyota huyu mwenye bao moja kati ya mawili ambayo Yanga imefunga.
Haruna Niyonzima
Mtambo wa mabao yote mawili yaliyofungwa na Yanga anawajua vizuri Simba kwa kuwa alishawahi kucheza huko msimu wa 2018/19.
Kibwana Shomari
Kijana huyu akiwa pembeni ni mwepesi kutengeneza na kuwaga maji. Licha ya kutoonekana sana kwenye Kombe la Mapinduzi ana tuzo ya mchezaji bora ambayo aliipata kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC.
Michael Sarpong
Mwili jumba ndani ya uwanja ikiwa mabeki wa Simba watampuuzia atawapa maumivu kwa kuwa ni miongoni mwa washambuliaji wenye juhudi ndani ya uwanja ila hana bahati.
Anakumbukwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliowakutanisha Uwanja wa Mkapa ambapo aliweza kuwafunga watani hao wa jadi kwa mkwaju wa penalti kwenye sare ya kufungana bao 1-1.
Wamefikaje
Safari ya Simba ilikuwa namna hii:-Simba 3-1 Chipukizi.
Simba 2-0 Mtibwa Sugar.
Simba 2-1 Namungo FC.
Yanga mwendo wao ulikuwa namna hii:-Yanga 0-0 Jamhuri.
Yanga 1-0 Namungo.
Yanga 1-1 Azam FC,(Penalti 5-4).
Ukuta wa Yanga ni kikwazo
Rekodi zinaonyesha kwamba kikosi cha Yanga ni imara kwenye ulinzi ambapo ndani ya dakika 270 ambazo ni mechi tatu imeruhusu kufungwa bao moja pekee ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Azam FC wakati ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 90.
Ukuta wake umeonekana kuwa imara chini ya Juma Makapu na Abdalah Shaibu, ‘Ninja’ ambao wamekuwa na maelewano kwenye mechi zote tatu.
Kwa upande wa Simba safu ya ulinzi chini ya Kenedy Juma imeruhusu mabao mawili kwenye mechi tatu ilizocheza.
Safu ya ushambuliaji Simba kiwembe
Safu ya ushambuliaji imeonekana kuwa imara ambapo imefunga mabao 7 kwenye mechi tatu ambazo wamecheza ndani ya dakika 270.
Ikiwa chini ya Meddie Kagere mwenye mabao mawili, kiungo Miraji Athuman yeye ametupia mabao manne huku bao moja likiwa ni mali ya Hassan Dilunga.
Kwa upande wa ile ya Yanga imetupia jumla ya mabao mawili na wamiliki wa mabao hayo ni Tuisila Kisinda na Zawadi Mauya ambao wote ni viungo.
Maneno ya makocha
Seleman Matola, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kwamba mchezo utakuwa mgumu kutokana na kila timu kuhitaji kupata ushindi kwenye mchezo huo.
“Kila timu inahitaji kupata ushindi hata wachezaji wangu wanajua, hivyo ninaamini kwamba utakuwa ni mchezo wenye ushindani mkubwa ila tutapambana kufanya vizuri,” .
Cedric Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ikiwa timu inashiriki mashindano inahitaji kupata kombe hicho ndicho anachokitarajia.
“Timu inashiriki mashindano ili kupata kombe ambalo inapambania. Ninawapongeza wacheaji kwa kupambana hivyo ni wakati wetu wa kufikia malengo ambayo tumejiwekea,” .
Wamekutana mara moja fainali
Kwenye Kombe la Mapinduzi hawa watani wamekutana mara moja kwenye fainali ilikuwa ni msimu wa 2011 ambapo Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na Simba.
Leo inakuwa mara ya pili ambapo kila timu inahitaji kusepa na taji hilo la heshima.
Vita ya rekodi
Simba inaingia uwanjani kusaka taji la nne la Kombe la Mapinduzi huku Yanga ikiingia uwanjani kusaka taji la pili la kombe hili.
Mjalibu kutafuta habari dah!
ReplyDelete