January 5, 2021


 KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa wamekutana na timu nzuri ndani ya Uwanja wa Amaan jambo lililowafanya walazimishe sare ya bila kufungana.

Mchezo wa leo wa Kombe la Mapinduzi ambao ni wa makundi ikiw ipo kundi A pamoja na timu ya Namungo umekamilika kwa dakika 90 kwa timu zote mbili zilizokuwa uwanjani ambazo ni Yanga na Jamhuri kutoshana nguvu bila kufungana.

Shukrani kwa kipa namba moja wa Jamhuri, Nasoro Twaliba ambaye alikuwa na kazi ya kuokoa mashuti ya Wazir Junior ambaye alikosa utulivu kipindi cha kwanza pamoja na Yacouba Songne ambaye naye alishindwa kupachika bao kutokana na uimara wa kipa wa Jamhuri.

Pia kipa wa Yanga , Farouk Shikalo naye alikuwa makini kulinda lango lake ambapo aliokoa michomo ya  Ally Juma pamoja na Yunus Makame ndani ya uwanja.

Kaze amesema:"Tumekutana na timu bora na imara jambo ambalo limefanya tupate matokeo haya, kwa kuwa ni mwanzo bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zetu zijazo," .

Mchezaji bora wa mchezo wa leo Juma Ally wa Klabu ya Jamhuri ya Zanzibar ambaye amepewa zawadi ya laki mbili amesema kwake ni furaha kuwa mchezaji bora na anaamini watazidi kupambana kwa ajili ya mechi zijazo.

7 COMMENTS:

  1. Ndio mtawpata ubingwa mwaka huu. Yetu macho tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwamba unataka kutuaminisha bingwa hawezi kupatikana kwa timu kupata sare? au unamaanisha nini mdau?

      Delete
  2. Ni kwa vile saido hakucheza, wangeyaoga hao

    ReplyDelete
  3. Na kwanini hakucheza.

    ReplyDelete
  4. Kocha naona umesema vizuri sana. Ila kuna shida kwa timu yako kutegemea mabeki kufunga na viungo ni hatari kwa mstakabali wa timu.

    ReplyDelete
  5. INAOEKANA KOCHA AMEISHIWA HATA MBINU, ANGALIENI SARPONG, KISINDA, YACOUBA, KIBWANA SHOMARI BADO TIMU IMESHINDWA KUBADILI MATOKEO...KUNA WACHEZAJI PALE YANGA HAWAFANANI NA MBINU ZA KOCHA, YAANI KOCHA ANAJITETEA KWA KUSEMA WACHEZAJI WAMETUMIKA SANA, TIMU INA WACHEZAJI 30 JE HAKUNA WENGINE AMBAO UKIPANGA UTAPATA MATOKEO MAZURI YENYE TIJA? JAMHURI TIMU YA DARAJA LA KWANZA LAKINI IMEWEZA KUWABANA YANGA NA SUB ZKE ZOTE, JAMHURI WALIANZA KUFANYA SUB BAADA YA YANGA KUMALIZA SUB ZAO

    ReplyDelete
  6. Saido kagomea hoteli, hawana imani na baadhi ya wachezaji.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic