February 15, 2021

 


BAADA ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kikosi hicho kimeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Mbeya City, utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Februari 18.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu,  George Lwandamina ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na ina pointi 33 kibindoni. 

Itawakaribisha Mbeya City iliyo nafasi ya 17 na pointi zao ni 15 wote wamecheza jumla ya mechi 19 ndani ya msimu wa 2020/21.

Walipokutana Uwanja wa Sokoine,  mzunguko wa kwanza,  Azam FC ilishinda bao 1-0 hivyo mchezo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa mipango yao ni kufanya vizuri kwenye mechi zao zilizobaki.

"Kushindwa kupata matokeo kwenye mechi iliyopita haina maana kwamba hatupo imara, benchi la ufundi litafanyia kazi makosa kisha tutaendelea kusaka ushindi kwenye mechi zetu zijazo," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic