February 18, 2021

 

 


KIKOSI cha klabu ya Azam leo kinatarajia kuikaribisha Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa katika dimba la Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam, huku wakiikosa huduma ya kiungo wao Mwandamizi, Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Azam inaingia katika mchezo huu ihuku ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 2-1 walichokipata kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Coastal Union.

Kikosi hicho kimekuwa kikipitia katika kipindi kigumu ambapo tangu mwaka huu uanze hawajashinda mchezo wowote, huku kumbukumbu ya mwisho ya ushindi kwenye ligi ni ule dhidi ya Polisi Tanzania Desemba 31, mwaka jana.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Mbeya City, Azam iliibuka na ushindi wa bao 1-0 mchezo uliopigwa katika dimba Sokoine jijini Mbeya Septemba 20, mwaka jana.

Akizungumzia mchezo huo, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Kikosi tayari kimefanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wetu wa kesho (leo) dhidi ya Mbeya City.

“Tunaingia katika mchezo huu tukiwa hatuna kumbukumbu nzuri ya mchezo wetu uliopita ambao tulipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union, tayari benchi la ufundi limeshafanya tathimini ya mapungufu tuliyoyaonyesha katika michezo iliyopita na tupo tayari kwa ajili ya kusaka ushindi.

“Kuelekea mchezo huu kikosi chetu kitakosa huduma ya nyota Salum Abubakar ‘Sure Boy’ ambaye amepata majeraha ya nyonga, lakini tuna faida ya kurejea kwa Obrey Chirwa, Emmanuel Charles, na Abdul Omary ambao waliukosa mchezo uliopita kutokana na kuwa na majeraha,”

Azam inakamatia nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi zao 33 kwenye michezo 19 waliyocheza mpaka sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic