February 18, 2021

 



UONGOZI wa klabu ya soka ya Namungo umesema kuwa maamuzi ya kamati maalum ya Shirikisho la soka Afrika (CAF), kuamua michezo yote miwili ya hatua ya mtoano dhidi ya Clube Desportivo 1º de Agosto ya Angola ipigwe hapa nchini ni faida kubwa kwao kwa kuwa watacheza katika mazingira waliyozoea.

Hatua hiyo imekuja muda mfupi baada ya Namungo kurejea nchini wakitokea Angola ambapo walikumbana na matukio mengi yasiyokuwa ya kimchezo, kiasi cha CAF kuufuta mchezo wa kwanza uliopangwa kufanyika nchini Angola Jumapili iliyopita.

Namungo ilirejea nchini siku ya Jumatatu bila wachezaji wake watatu na Ofisa Mtendaji mkuu wa kikosi chao, ambao walitajwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.

Uamuzi huo wa kamati maalum ya CAF iliyokuwa ikishughulikia sakata hilo umekuja baada ya kubainika kuwa si wenyeji de Agosto wala Namungo, iliyohusika moja kwa moja kukwamisha mechi ya kwanza hivyo kuamuru mechi zote mbili kuchezwa angalau ndani ya saa 72, na ziwe zimechezwa kufikia Februari 26.

Agosto watakuwa mwenyeji wa mechi ya kwanza, huku Namungo wao wakiwa wenyeji kwenye mchezo wa pili.

Akizungumzia maamuzi hayo, Ofisa habari wa Namungo, Kindamba Namlia amesema: “Maamuzi yaliyotolewa na Shirikisho la soka Afrika, (CAF) tumeyapokea, na hatuwezi kuyalalamikia kwa sababu wao wamefanya tathimini ya kile ambacho kilitokea Angola na kuja na maamuzi hayo.

“Jambo zuri ni kwamba wakati huu sisi tutakuwa nyumbani, kimazingira hii ni faida kwetu na kikosi tayari kimeanza mazoezi tangu Jumanne kuelekea mchezo wetu wa kwanza ambao tutacheza Februari 21, hatuna majeruhi yoyote na kuhusu mchezo wa marudiano sisi tutajua ni lini utachezwa,”

 

 

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic