February 12, 2021


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa haukuwa na chaguo la kufanya Uwanja wa Mkwakwani jana kwa kuwa uwanja haukuruhusu wacheze mipira ya chini jambo ambalo liliwafanya wapoteze pointi tatu.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ilikubali kuacha pointi tatu zote baada ya kufungwa mabao 2-1.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa aliongea na mwalimu na kumuuliza tatizo lipo wapi mwalimu aliweka wazi kwamba uwanja ulikuwa tatizo kwao kuwa haukuruhusu mipira ya chini.

"Haukuwa uwanja rafiki kwetu kwa kuwa ulikuwa hauruhusu mipira ya chini jambo ambalo limetufanya tushindwe kupata matokeo chanya ndani ya uwanja.

"Ukiangalia kwa takwimu vijana wetu walipambana na kufanya vizuri ila wapinzani wetu waliweza kupiga mashuti mawili yaliyolenga lango na wakashinda hivyo tunajipanga kwa ajili ya mechi zijazo,".
 

7 COMMENTS:

  1. Upuuzi mtupu, eti tatizo uwanja, kwan ni mara ya kwanza Azam kucheza mkwakwani? Siku zingine walikuwa wanachezaje? Ndio kusema viwanja vyote "vibovu" watashindwa kucheza na kutopata matokeo?

    ReplyDelete
  2. Zakazaka tuliza mdomo wako huo ndio mpira ulivyo na ukubali kushindwa. Mbona ile mechi iliyopita haukumwuliza mwalimu mlipataje share ukakimbilia kutoa tathmini yako sasa leo umekutana na matokeo sio rafiki unamtafuta mchawi. Kubali tyuu mchezo wowote ule una matokeo matatu na haijalishi unachezwa kwenye mvua, tope nk....

    ReplyDelete
  3. Ila ule uwanja sijui waliufungulia kwa vigezo gani ingawa sikubaliani na sababu za azam

    ReplyDelete
  4. Walipotoka sare na Simba wakajua ligi imekwisha. Sifa za timu ndogo zimeikumba Azam .Kukamia mechi.Kila mechi ni pointi 3.

    ReplyDelete
  5. Kwani walioshinda(coastal) walitumia uwanja gani,,,lazima kocha na wachezaji wabadilike kulingana na mazingira,,,ukisema viwanja vibovu huku unataka ubingwa ni vichekesho,,,angalia wenzao utopolo,,,nyau,,,wanapambana popote,,,ushororo na ufundi lazma uongezeke au upungue kulingana na uwanja,,,bac wawajengee viwanja timu zingine ili wacheze mpra wao wa chini

    ReplyDelete
  6. Msemaji apunguze mdomo aliongea Sana alipopata sare na Simba aache visingizio

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic