Beki huyo wa kulia ni mmoja wa manahodha wa kikosi cha AS Vita ambapo licha ya kuwa ni beki wa kulia lakini ndiye kinara katika utupiaji wa mabao katika kikosi cha AS Vita katika Ligi Kuu ya Congo mara baada ya kufunga mabao matano katika ligi hiyo msimu huu huku akiwapita baadhi ya washambuliaji wa timu hiyo.
Mmoja kati ya wachezaji wa kikosi cha AS Vita ambaye ni rafiki mkubwa wa beki huyo ambapo wote walicheza katika mchezo dhidi ya Simba, amesema kuwa ameambiwa na mchezaji huyo viongozi wa Simba wameanza kuulizia uwezekanao wa kumsajili mchezaji huyo mwisho wa msimu huu.
“Djuma ni rafiki yangu, tumekuwa wote AS Vita kwa muda sasa na wote ni manahodha katika kikosi hiki, ameniambia kuna viongozi wa Simba wanamfuatilia kwa ajili ya uwezekano wa kusajiliwa mwishoni mwa msimu huu, sijajua yeye kwa upande wake ataamua nini na anafikiria nini kuhusu Simba,” alisema kiungo huyo.
Simba licha ya kumuhitaji beki huyo ambaye anacheza upande wa beki wa kulia, katika nafasi hiyo wapo Shomari Kapombe na David Kameta ‘Duchu’.
Lemgo kubwa ni kuongeza nguvu kwa upande wa beki ili kuongeza nguvu sehemu ya ulinzi kuwa imara zaidi hasa kwenye mechi za kimataifa ambazo ushindani wake ni mkubwa.
Kijana anaujua mpira haswa ,,aje tu msimbazini.
ReplyDeleteShabani ni mchezaji haswa ila sidhani kama wanaweza kushindana na vilabu vyenye nguvu zaidi ndani na nje ya bara la Africa kuipata saini yake. Ni mchezaji klabu yeyote ya Africa yenye malengo ingetamani kuwa nae hata kwa record signing fee.
DeleteMmeshaanza kumrubun, nawashaur as vita wasimpange tena huyu beki itakuwa kama kwa chikwende sasa
ReplyDeleteVisingizio FC AKA malalamiko FC Kila wanachotaka kufanya Simba lazima walalamike Yani tumrubuni kwa lipi hasa tumecheza nao kwao uwanja wao ambao hawajafungwa karibu mwaka mzima tumewafunga tuje kumrubuni akija hapo Taifa tatizo washabiki wengi wa Yanga mmekalia propaganda na kuzusha vitu ambavyo havipo ili kuidhoofisha Simba na ndio Mana hamuendelei,nyie endeleeni na propaganda sijui marefa wanawaonea sijui Mara TFF yote Simba,sijui Simba wanacheza mechi zetu so tunazidi kuchanja tu kimataifa nyie bakini hapo hapo kwenye kuwapokea wapinzani wa Simba na kuwatafutia hifadhi
DeleteAhahaha
DeleteImekuumiza Sana we
ReplyDeleteSimba ndio timu inayojuwa kuchaguwa nyota wa kazi. Simba huchaguwa kimyakimya bila ya kelele na majigambo kwa kuwaita machine za magoli na nyota wenyewe kudai kazi yetu ni kutia magoli na mwisho wa siku Kumbe hawana chochote. Nyota wa kweli hataki muda wa kuzoweana kama akina Kagere, Konde Boy na wengineo siku ya kwanza Kagere alitia goli
ReplyDeleteSiku hizi jamaa kimya kuhusu kuleta mashine mpya za magoli na Mnyama mwenyewe anapomtaka nyota ambaye kwahakika arazudu kuipaisha juu timu kutokana na hasadi zao kama wa huyo hapo juu anasema "wameshaanza kumrubuni". Zile harakati zao za kila siku za kuwarubuni wachezaji wa Simba sasa zimekufa Fofofoooo
ReplyDeleteHivi huyu beki Shabani Djuma ana umri gani... Anaejua anisaidie
ReplyDeleteMIAKA 27 MZEE , AMEZALIWA MARCH 16, 1993
Deletemiaka 34
ReplyDeleteUMEANGALI PLAYER PROFILE YAKE MDAU?
DeleteKWA SUALA LA KUVUNJA MKATABA SIMBA ITASHINDWA, AS VITA WAMETUZIDI UCHUMI. KAMA WATAMUWAHI MKATABA WAKE UKIISHA WANWEZA KUMPATA KWA BEI CHEE, LAKINI IATEGEMEA NI TIMU GANI PIA ZIMEPELEKA OFA NZURI KWAKE. HILI SUALA NI KAMA LA WALTER BWALYA. WALTER ALIKUWA MCHEZAJI WA KAWAIDA SANA AND EVEN NOW AKIWA AL AHLY. LAKINI NKANA RANGERS WALIDAI DOLA LAKI 400. NANDIYO HIZO HIZO AL AHLY WALILIPA KWA NKANA RANGERS. AL AHLY WAMEIZIDI SIMBA KWA UCHUMI. KIKOSI CHA AL AHLY KINA THAMANI YA EURO MILIONI 25.5 NI SAWA NA BILIONI 71.66 ZA KITANZANIA.
ReplyDeleteal ahly hawakumnunua bwalya kutoka nkana mzee bwalya kuna timu ya hapo misri ndo ilimsajiri na al ahly ndo wakamchukua
DeleteSawa kabisa,Ila mpira Ni uwekezaji na Simba ndo timu pekee Tanzania iliyo na uchumi mzuri kwa Sasa.
ReplyDeleteSawa Ila Simba wanaweza kwa sasa
ReplyDelete