SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeamua mechi zote mbili za Kombe la Shirikisho kati ya CD 1 Agosto ya Angola na Namungo FC ya Tanzania zichezwe nchini Tanzania.
Uamuzi huo umefanywa baada ya Kamati ya CAF ya Mashindano hayo kubaini kuwa si Agosto wala Namungo iliyohusika moja kwa moja kukwamisha mechi ya kwanza iliyokuwa ichezwe Februari 14 nchini Angola.
Mechi zote mbili zinatakiwa kuchezwa angalau ndani ya saa 72, na ziwe zimechezwa kufikia Februari 26 mwaka huu.
Kwa mujibu wa ratiba, CD 1 Agosto itakuwa mwenyeji wa mechi ya kwanza, hivyo itawajibika katika maandalizi yote ikiwemo gharama za maofisa wa mechi hiyo.
Kwa vile makundi ya Kombe la Shirikisho yatapangwa Februari 22, mshindi wa jumla baada ya mechi hizo mbili hatazingatiwa katika viwango (non-ranked) wakati wa upangaji.

Mechi hiyo iliahirishwa kwa kile ambacho kilielezwa kuwa mamlaka ya Angola iliwataka wachezaji wote wawekwe karantini baada ya wachezaji watatu pamoja na kiongozi mmoja wa Namungo kuelezwa kuwa wamekutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona.
Baada ya Namungo kugomea jambo hilo mamlaka ya Soka ya Tanzania, (TFF) walifuatilia kwa pamoja ili kupata ukweli wa mambo mpaka pale Caf ilipoamua kufuta mchezo huo wa kwanza ugenini.
Hivyo kwa taarifa iliyotolewa na TFF leo Februari 17 ni rasmi Namungo atakuwa nyumbani kwenye mechi zote mbili ndani ya Bongo.
Nafasi ya dhahabu hiyo kwa Namungo, Allah awape nini kingine???
ReplyDeleteHuku ndio kuruka mkojo unakanyaga kinyesi
ReplyDeleteHahahahaha nimefurahi sana, cha msingi mashabiki tuujaze uwanja, tuwape sapoti wafanye vyema.
ReplyDeleteSasa wameingia kule tulipokuwa tunapataka.Ihakikishwe wachezaji wao saba wana Corona halafu wapelekwe kambini JKT Ruvu wakakae karantini ya wiki mbili.Ukimwaga mboga mi namwaga mchanga kwenye ugali
ReplyDeleteUKIMWAGA MCHANGA KWENYE UGALI ANAWEZA KUUOSHA NA MAJI, HIYO TIMU INAYOCHEZA NA NAMUNGO SIO YA KUBEZA. UNAWEZA SHANGAA NAMUNGO ANAPIGWA HAPA HAPA KWAO. KIKUBWA NAMUNGO AJIANDAE KWA HALI NA MALI NA SIO VINGINEVYO. NCHI BADO HAINA MASHABIKI WAKUFANYA FIGISU FIGISU ZA SOKA, INA MASHABIKI WENYE UPENDO NA AMANI. NI JUKUMU LA NAMUNGO KUFANYA VIZURI NA SIO MASHABIKI
Delete