February 22, 2021

 


NYOTA wa Al Ahly, Walter Bwalya amesema kuwa wamekuja Dar kwa lengo moja la kusaka ushindi mbele ya Simba kwenye mchezo wao wa hatua ya makundi ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Al Ahly ambao ni wababe wa soka ndani ya Afrika wakiwa ni washindi wa tatu kwenye Klabu Bingwa Duniani wanatarajiwa kumenyana na Simba, Uwanja wa Mkapa, Februari 23.

Kwa sasa kwenye kundi A, Al Ahly wanaongoza kwa idadi ya mabao matatu huku Simba wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi tatu baada ya kufungua pazia kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita, mchezo uliochezwa DR Congo.

 Bwalya amesema kuwa wanawatambua vizuri wapinzani wao hivyo hawatawapa shida kupata matokeo ndani ya uwanja.

“Tunawatambua Simba uimara wao na pale ambapo wanakosea hivyo tumekuja Dar kwa lengo moja la kusaka ushindi na hilo linawezekana kwa kuwa tupo imara.

“Nitapambana nami pia kuweza kuifunga Simba ili kuweze kufanikisha malengo ya Klabu ambayo ni kutwaa ubingwa wa Afrika,” amesema.

Bwalya aliibuka ndani ya kikosi hicho akitokea Klabu ya Nkana ya Zambia na iliwahi kucheza na Simba kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa ilitolewa Uwanja wa Mkapa hatua ya mtoano kwa kufungwa mabao 4-3.

Walipokuwa nyumbani, Nkana ilishinda 2-1 na zilipokuutana Uwanja wa Mkapa, Simba ilishinda mabao 3-1. 

8 COMMENTS:

  1. Usiongee sana w.bwalya watakuambia kuwa una corona

    ReplyDelete
    Replies
    1. AS VITA WALIKUWA WAMETIMIA PALE SAWA? HUYU BWALYA NDIYO NANI? ALIKUJA AMRI WADAR, HOSAM HASAN GHAL, WAKINA ABOUTRIKA, MUHAMMAD BARAKAT, HUYU NDIYO NANI? NI PIMBI TU KATIKA ARDHI YA TANZANIA. MUULIZE KAFUNGA AMGOLI MANGAPI TANGU ATUE AL AHLY? KAGERE KAIFUNGIA MAGOLI 8 MPAKA LEO SIMBA KATIKA LIGI. HUYU BWALYA KAIFUNGIA AL AHLY MABAO MANGAPI MSIMU HUU WA 2020/21?

      Delete
  2. Alifungwa wakati alipocheza dakika 90 na mpk akatoa machozi. Ebu kumbuka zile goli 3 zilizomliza

    ReplyDelete
  3. Huyo refa Mkenya aliyewasaidia kushinda mpaka leo kapotea au umesahau dk 1 anampa yellow card left back wa Nkana eti kachelewesha mpira bila kusahau goli la Chama faulo badala iende Simba inaelekezwa Nkana wt Wana mhoji refa Wahuni wanaanza mpira goli.Na ule mchezo ulikuwa na maelekezo kwa refa kijumla

    ReplyDelete
    Replies
    1. AISEE YANGA AWE BINGWA NA NYIE MSHINDE ZENU ZOTE KLABU AFRIKA KELELE ZIISHE

      Delete
  4. Kipigo kwa kwa Waarabu na kikundi cha ushangiliaji cha Utopolo kipo palepale kwa Mkapa hatoki mtu , huyu si ndio alilia game na Nkana kilio kingine kinamuhusu This is Simba

    ReplyDelete
    Replies
    1. SAFARI HII ILE TIMU YA KUFUNGWA 5 HAIPO TENA. DK 90 ZIKIISHA ATASEMA NATAKA KUBAKIA SIMBA. MAANA WALTER BWALYA PALE AL AHLY SIO MTU TEGEMEO. TAKWIMU ZINAONGEA.

      Delete
  5. Maneno yote majibu yatapatikana leo uwanjani, lkn Tukumbuke anaejua Anajua tu, Al Ahly ananafasikubwa ya kushinda...!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic