February 19, 2021

 



Na Saleh Ally

MOJA ya sifa kubwa za wapenda mpira ni kutokuwa wakweli, kutopenda kuelezana ukweli na kupendelea kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa!



Bahati mbaya zaidi wale ambao hupenda kuwa wazi au kusema ukweli, ndio huonekana wabaya kwa kuwa soka ni mchezo uliozungukwa na watu wengi wanafiki ambao kazi yao ni kusema maneno ya uongo ili waishi.



Haiwezekani kukawa na mabadiliko kwenda katika mafanikio kama watu wataona kusema uongo au unafiki kuwapamba watu na kadhalika ndio maneno sahihi yanayoweza kuleta mabadiliko au mafanikio.


 Nimeona juzi, Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla akitolewa Uwanja wa Mkapa huku baadhi ya mashabiki wakisema maneno makali dhidi ya uongozi wa Yanga.



Mashabiki hao wameonyesha kukerwa na kikosi cha Yanga kupata sare ya nne mfululizo katika mechi yao dhidi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.



Walipata sare dhidi ya Gwambina na Tanzania Prisons katika mzunguko wa kwanza, kisha kwenye mzunguko wa pili wakapata sare ya kwanza ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City wakiwa ugenini jijini Mbeya na hii ya juzi ya mabao 3-3 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, maana yake ndani ya mechi mbili, Yanga wamendondosha pointi nne.



Wako kileleni lakini wanajua kiasi gani wanahatarisha uongozi wao dhidi ya mabingwa watetezi, watani wao Simba ambao kama watashinda mechi tatu zilizobaki za viporo, wataizidi Yanga kwa pointi mbili na mabao ya kufunga pia.



Wakati mashabiki wakionekana kuudhiwa na hilo, hasira zao zinakwenda moja kwa moja kwa Dk Msolla kwa kuwa wanajua ndiye walimpa dhamana ya kuiendesha klabu yao, wana haki.



Hasira za kwamba kuna jambo haliendi vizuri na mhusika mkuu ni Dk Msolla. Kwangu taratibu naanza kujiuliza, kweli Dk Msolla anasajili? Tumewahi kuona akileta wachezaji na kuwasainisha? Jibu litakuwa hapana na ukweli hiki ni kitu Yanga wanakikosea na huenda watakasirishwa na kuambiwa lakini utafikia wakati watajifunza kupitia ninachoandika.



Ukiangalia kwa undani unaona kwa kiasi kikubwa Dk Msolla pamoja na uongozi wake wanakosea, kiasi kwangu naweza kuhoji kwamba leo tunaweza tukawauliza usajili wao? Maana usajili wa Yanga unafanywa na wadhamini na si klabuni.



Usajili wa Yanga, unafanywa na nani? Sote tunajua na unaona viongozi hawashiriki na kama wanashiriki, wapi? Maana hata wakati wachezaji wakisajiliwa, wamekuwa hawaonekani na mara nyingi usajili haufanyiki katika klabu hiyo. Mara nyingi tunawaona wakiwa na wadhamini na si viongozi wanaohusika.



Lazima Wanayanga wawalalamikie viongozi au kuwalaumu kwa kuwa ndio waliowapa dhamana, sahihi. Lakini tujiulize, viongozi wanashiriki katika kilicho sahihi kwa maana ya klabu kwamba wanajua au kufanya kila kinachotakiwa?



Binafsi naona wadhamini wao wana nia nzuri lakini ukweli lazima viongozi wa klabu wawe na nguvu sahihi ya ushiriki wa mambo.



Unaona leo mashabiki wanalia na wao kwa kuwa wanajua ndio wanaofanya kila kitu. Ndani ya klabu wanashiriki yote, wao ndio wanaamua yote au hawana nguvu tena na uamuzi unafanywa na wengine.



Nimekuwa nikiiona shida Yanga hapo baadaye, ninaona watu wakitupiana lawama na ikiwezekana wadhamini kukwazwa jambo ambalo kama utaratibu mzuri utafanyika mapema unaweza kuokoa mengine yasiyo sahihi kutokea mbele.



Msiwaache Dk Msolla na Frederick Mwakalebela wawe watu wa kulaumiwa tu mwishoni lakini wakati wa utendaji wakawa wanafanya watu wengine wa kamati au wadhamini.



Dk Msolla na Mwakalebela, wote ni wazoefu katika mpira na ndio wana dhamana ya wanachama na mashabiki, basi wasimamie kile ambacho wamekabidhiwa kwa ubora ulio sahihi badala ya kufanya mambo ili mradi tu.



Nimesema mwanzo, hatuambiani ukweli na wengine wanahofia kusema watawaudhi watu fulani lakini ukweli ni hivi, Yanga ni timu ya Watanzania na tunapaswa kuambiana ukweli mambo yaende sawa kwa kuwa maendeleo ya klabu hiyo kongwe ni maendeleo ya mpira wa Tanzania.


 



22 COMMENTS:

  1. Utaniambia mwandishi kama kweli wewe ni mkweli.Simba walipofungwa na Ruvu shooting, na prison, alilaumiwa nani? Nani wale walipofungwa? Je,walihusika usajili wa mikia? Yanga umetoka kuishinda mechi nyingi tu,unasema kikosi kimesajiliwa vibaya? Wanachohoji watu ni kwa nini ghafla timu icheze vibaya? Late majibu kama huna wewe ni mnafiki.tuachie timu yetu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu Saleh Jembe mbabaishaji sana! Bogus sana!

      Delete
  2. Hakuna short cut kwenye mafanikio mnalazimisha furaha nyie utopolo wekezeni Simba is too far maana rahisi next lever

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uwekezaji wa Simba ni upi wakati bado mnatupimia pesa ya mdhamin na sio ya mwekezaji

      Delete
  3. Kwanini brother mnapenda kukuza Mambo,kwa kisingizio Cha Tathnia, ni kweli Yanga inaongoza Ligi na ipo kileleni na ni mafanikio ,naomba ukubali kuwa unataka kuendelea kutumia fani yako na mahaba yako kuivuruga Yanga hili upande unaoupenda unafaike kwa maana wao wakiteleza umekuwa na vitabu virefu vya kuimanisha ,ninayo Magazeti ya Champion na S Extra ya miaka Kadhaha ,.Nasoma makala zako nyingi umekuwa mediator pale Simba inapoonekana kuvurugikiwa ukiwapa moyo,Lkn kwa Yanga unachochea mgogoro unaandika ki umbea, Kuna makala Sijui kupiga waamuzi au kwenda na matokeo uwanjani siyo kwa mpira wa sasa,huku Msolla hajasajili.Lakini Mimi kwa uelewa wangu najua umelenga nani ambaye ni Tishio kwa hisia na upande wako ambaye ni GSM na Mambo yake .Kwa maana mafanikio ya Yanga unakuwa sehemu ya kuharibu Umoja hachana na enzi za Friends of Simba.

    ReplyDelete
  4. Na Elimu mliyo nayo kwamba Mkiti wa Timu kazi yake ni Nini na majukumu yake no yapi kwa mujibu wa Katiba ya Yanga?Na GSM kaletwa na Nani Yanga?HV niulize ni kweli Mh Magufuli kila analofanya linafanikiwa,na je Kati ya aliyofanya na anayofanya Mengi si ni +,na je hakuna Watu wanaosubiri kosa wamlaumu? na je wanaandikwa na kutangazwa hadharani na kuonekana wana hoja Kama siyo taarifa za kusifia na kupongeza tu.

    ReplyDelete
  5. Anzisha Blog ya Simba tujue mkuu

    ReplyDelete
  6. Hivi soka la bongo kwani nilazima Simba au Yanga ndo ziwe zinashinda siku zote,Yanga wajipe muda Simba wamewekeza zaidi ya yanga na kwa muda mrefu na bado wanafungwa,Yanga wao kutoa drow imekuwa shida kubwa mjini je siku watakapo fungwa itakuwaje,Uwekezaji waliofanya Yanga mwaka huu na mwaka huu huu wanautaka ubingwa kwa fujo zote hizo...dah hilo ndo soka letu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Eti uwekezaji! Hivi unajua maana ya uwekezaji wewe? Billioni 20 sio biriani 20! Ni ubabaishaji mtupu! Ni umbumbumbu tu unamnufaisha "mwekezaji". Zingatia hayo mabano, nitafute baada ya miezi 6.

      Delete
  7. Ni mwanzo huo. Bahati hawajamchania nguo
    Hiyo ndio tabia ya gongowazi na wala hapatikani kwengineko. Tukana, zomea, chana na piga

    ReplyDelete
  8. Eti nitafute baada ta miezi 6.Utopolo wana ngebe lakini vitendo.Mafanikio hayalazimishwi.Timu bado mbovu. Nugaz amewaasa acheni kwenda na matokeo mfukoni.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tujikite kwenye hoja yako ya uwekezaji. Unajua maana ya uwekezaji? Mbona hujibu swali? Nionyeshe kitega uchumi kimoja tu cha Simba, ukiachilia mbali kile kiwanja cha mazoezi Bunju! Hivi sasa makao makuu ya Simba yako wapi? Popo tu wamejaa pale Msimbazi! Hata kupaka rangi kumewashinda! Unazifahamu Mo Simba (Mind you ule uwanja wa Bunju unaitwa Mo Simba Arena) na Simba Holdings? Muulize Magori na fuatilia records zilizopo FCC. Ati uwekezaji! Mark my words, utakuja kumkumbuka mzee Kilomoni.

      Delete
    2. Ukitaka mafanikio usijilinganishe na mwenzako hautapiga hatua kamwe

      Be u're self

      Delete
    3. Zezeta usidandie hoja usiyoifahamu. Nani anayelinganisha hapa? Hapa ni hoja ya uwekezaji. Nini maana ya uwekezaji?

      Delete
    4. Tokea Manji awakimbie mmekuwa na stresses na mmebaki kujifariji kwa ndoto za Abunuwasi. Utopolo a.k.a Malalamiko FC ni sawa na debe tupu ambalo haliachi kupiga kelele.

      Delete
  9. Mimi nataka TCRA Anonymous,Uknown na ma nickname Mengi yanayotumika yakomeshwe hapa Kuna behind the scene inaendelea,hata Mimi nimependa Ile tafsiri ya Uwekezaji wa 900M kwenda 4.5B na uhalisia wa Uwekezaji kwa Ujumla.Kwahiyo yule Sheikh wa Saudia ,alipotapka kuwekezaka Newcastle Paundi B300 plus ilikuwa ni kusajili?tuache mahaba

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hii safi ili yale mautopolo yanayomwaga mitusi yabainike

      Delete
  10. Utopolo mtuambie kitendo cha msola kusakamwa ni sahihi? Kama ndiyo usahihi wake ni upi?

    ReplyDelete
  11. Kijana Msolwa anasakamwa na Simba Timu,JIONGEZE hata hao wanao rushwa kwa you tube ni utapeli wenu Mikia ,endelea

    ReplyDelete
  12. Timu haijapoteza mchezo hata moja unaazaje kusema haifanyi Vizuri? Shida ninyi Waandishi wa Habari wa Mikia, ndiyo zenu....

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic