February 21, 2021


 GUU la kulia la nyota wa Simba, Bernard Morrison ambaye ni ingizo jipya ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Didier Gomes, raia wa Ufaransa linakera zaidi ndani ya uwanja kwa kuwa limehusika kwenye mabao matano kati ya sita ambayo amehusika nyota huyo.

Morrison ambaye aliibuka Simba na kusaini dili la miaka miwili amehusika kwenye mabao sita kati ya 42 yaliyofungwa na timu hiyo. Ni pasi moja ya bao alitoa kwa guu la kushoto ilikuwa Uwanja wa Mkapa.

Pasi ya kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara alitoa Uwanja wa Mkapa ilikuwa mbele ya Gwambina FC wakati Simba ikishinda mabao 3-0 kwa guu la kushoto dakika ya 90+3.

Bao lake la kwanza alifunga dakika ya 45+2, alitoa asisti ya pili dakika ya 28 ilikuwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati Simba ikishinda mabao 7-0 dhidi ya Coastal Union na alitumia guu la kulia kwa pasi na kufunga pia.

Bao lake la pili alifunga dakika ya 66 na alitoa pasi yake ya tatu zote kwa guu la kulia, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Simba ilishinda mabao 2-1.

Bao lake la tatu alifunga mbele ya Biashara United, Uwanja wa Karume,Mara wakati Simba ikishinda bao 1-0 na kusepa na pointi tatu na alitumia mguu wake wa kulia.

Morrison amesema:”Ninaipenda kazi yangu na ninapenda kuona tunapata mafanikio ndani ya uwanja, hivyo tutazidi kupambana ili kupata matokeo chanya ndani ya uwanja,”.

Februari 23 Simba ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Al Ahly ikiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, saa 10:00 jioni.

3 COMMENTS:

  1. Yupo vizuri licha ya kifanyiwa figisu nyingi za ndani na nje ya uwanja.

    ReplyDelete
  2. Tabu kila akifunga kesi yake na Utopolo inafufuliwa.
    Ila sasa nguvu kama imepungua wanadai pesa sio mchezaji. Huku mchezaji akidai hakuchukua pesa kutoka kwa Utopolo.

    ReplyDelete
  3. Upande WA pili majungu ndo mengi,NA lazima awakeleee mpka basii.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic