February 14, 2021

 

 

BAADA ya kuchezea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Simba kocha mkuu wa AS Vita, Florent Ibenge ameukubali mziki wa Simba kwa kusema kuwa wapinzani wao hao walikuwa bora zaidi katika mbinu.

AS Vita ikiwa nyumbani katika uwanja wa, Des Martrys de la Pentecote walipoteza dhidi ya Simba kwa kufungwa bao 1-0 lililofungwa kwa njia ya penati na mshambuliaji wa Simba Chris Mugalu.

Akizungumzia ubora wa Simba katika mchezo huo, kocha Ibenge amesema kuwa timu yake haikuwa bora.

“Timu yangu haikuwa bora dhidi ya wapinzani wetu, Simba walifahamu namna gani ya kucheza na sisi wakiwa ugenini, hivyo ubora wa wachezaji wangu ulikuwa chini katika kupangua mbinu za Simba.

“Nawapongeza wapinzani wetu kwa hilo lakini bado kuna safari ndefu japo si njema kupoteza tukiwa nyumbani, tunahitaji kuboresha ili tujiweke katika nafasi nzuri katika kundi letu,” alisema kocha huyo.

 

 

 

 

5 COMMENTS:

  1. Kashavuta fedha nzuri kutoka kwa manyau fc....achana na mbinu na mikakati ya wadaawa fc

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kawaida yenu utopolo madera yamewafanya mmekuwa wambeya wambeya

      Delete
  2. Simba inafedha ya kumuhonga Vita Club? Wabongo acheni kuhara kwenye midomo yenu.Hata Ahly nae akifungwa na simba itakuwa wamevuta fedha? Watu wa Yanga hamuwezi kuifanya Yanga ionekane bora kuliko simba kwa majugu na maneno ya kuzusha kwa simba kwani mpira ni mchezo wa hadharani na mpira unahitaji huduma pia kwa wachezaji. Yanga wapo hatarini kushushwa daraja kwa kushindwa kulipa million 40 za tambwe? Halafu wana ndoto ya ubingwa? Angalia wataalam wa benchi la simba tu halafu utajua kwanini simba inafanya vizuri Africa.

    ReplyDelete
  3. Hawa utopolo sijui wamesibiwa na nini. Hata mechi isiyowahusu ndewe wala sikio iliyopigwa Kinshasa wanatia midomo yao kwa kusema pesa imetumika. Hawa waliamini kabisa kuwa Mnyama atashindwa kama walivoshindwa wao na African Sports na Mbeya city

    ReplyDelete
  4. Iv kwel utakubal kuhongwa kwa ela iyo na upoteze kombe la clab bingwa lenye hela kubwa. Uto Tumien akili kuongea na cio matako

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic