February 22, 2021


 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wale wanaoibeza kazi yake waendelee kufanya hivyo kwa kuwa yeye anajua kile anachokifanya na kushindwa kupata matokeo kumemfanya atambue tabia halisi za Watazania.

Kwenye mechi zake mbili mfululizo za mzunguko wa pili, Kaze alikiongoza kikosi hicho kwa kuambulia pointi mbili wakati alipokuwa akisaka pointi sita na kushudia nyavu zake zikiguswa mara nne sawa na idadi ya mabao ambayo alifunga.

Alianza na sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine Mbeya, aliporejea Dar akakutana na sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wake wa tatu alishinda bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa kwa bao la Carlos Carlinhos.

Kaze amesema:"Sikuwa kwenye wakati mzuri hasa baada ya kutopata matokeo mazuri ndani ya uwanja na jambo hilo lilinifanya nijue tabia za Watanzania kwa kuwa wengi wanapenda kuongea.

"Labda niseme kwamba ikiwa utanibeza uwezo wangu mimi sawa kwa kuwa ninajua ninachokifanya ila sikuwa kwenye wakati mzuri wakati wa matokeo haya mabaya.

"Nimeona kuna watu wanajiita wachambuzi walikuwa wanasema kwamba nimeishiwa mbinu, sijui nini na nini, mambo mengi kweli wameongea," .


6 COMMENTS:

  1. Tatizo hata wewe mwenyewe unaongea mno

    ReplyDelete
  2. Kaze hii ndio bongo buana na ukumbuke wewe mwenyewe ndio uliwaaminisha kuhusu uwezo sasa usilikwepe hilo. Isitoshe mbona ligi bado sana wewe tulia tuu ili uone timu zinavyokamiana awamu hii ya lala salama... Punguza maneno acha visingizio wachambuzi hao hao ndio waliokusaidia kukuamsha kutoka kwenye kulewa sifa lkn leo hii unawabeza. Mwinyi Zahera alitoa mpk hela yake mfukoni kuisaidia timu lkn kwa sasa hayupo, ila wewe umezungukwa na lundo la wafadhili na bado ulichechemea. Wananchi wanataka matokeo sio porojo, kumbuka hata timu ya Taifa kuna mtu kaondolewa hivyo jiandae kisaikolojia...

    ReplyDelete
  3. Kaze akubali kukosolewa na kushaurika. Lilikuwa kosa kubwa sana kumtoa Kocha Mwambusi! Ni mzoefu wa ligi, ndani ya Yanga na fitna za kibongo. Sijui ulimwona jama adui au mpinzani kila anapokusahihisha husysan imani tako kwa baadhi ya mastaa waliochemsha! Nizar uliyenchagua hakufai wajati wa shida kama huu hana uzoefu wa ukocha kwa nfazi ya timu kama Yanga.
    Pia kimaamuzi unachelewa sana kufanya mabadiliko ana mchezaji anapishindwa kuendana na mchezo au mbinu zinapokwama.
    Wachambuzi sio adui zako ni site mirrors tu

    ReplyDelete
  4. Ni ukweli usio pingika bongo wajuaji ni wengi sana kila mtu anajifanya kocha pili kila timu inapokuja kucheza na Yanga au Simba hutumia nguvu nyingi sana wasifungwe lakin baada ya hizo mechi tena utaona matokeo yake hufungwa goli nyingi sana utashagangaa ule uwezo wao umeishhia wapi ni kwa ajili ya timu kubwa tu?

    ReplyDelete
  5. Niliwahi kusema Michael Sarpong utaondoka nae, narudia kusema hakika na kweli utaondoka nae, maneno yangu hupingwa na kubezwa hata na viongozi wa Yanga lakini mwishowe ufanya kile nilichotabiri, sijawahi kusema kitu kisitimie, mkataba wa Sarpong utavunjwa na wa kwako pia, mechi alizocheza Sarpong na utakazo mchezesha ndizo zilizochangia Yanga kupoteza points nyingi, na kuondoka katika nafasi ya ubingwa, Yanga itaishia nafasi ya 3 kwenye ligi kuu na kwenye FA itaishia mikononi mwa Azam fc nusu fainali, tatizo lako hushauriki na huwa amini wasaidizi wako, kuwa na cheti kikubwa si utendaji mzuri, ushirikiano na usikivu kwa wanao kuzunguka ndio vitu vinavyoweza kufanya cheti chako kikubwa kipate heshima zaidi. Pitso Mosimane ana cheti kikubwa lakini moja ya sifa kuu aliyo nayo anasikiliza sana ushauri wa wale wanaomzunguka katika benchi lake la ufundi ikiwa ni pamoja na wachezaji waandamizi. Kaze badilika mapema ondoa ushikaji na Sarpong, jamaa atakugharimu sana, hizo milioni 23 unazopata kila mwezi zitayeyuka Brother, GSM atashindwa vumilia kutoa mil 23 na kumlipa Sarpong zaidi ya mil 7 kila mwezi halafu mwisho wa mashindano timu ishike nafasi ya 3 na hata kombe la shirikisho ilikose, jua Senzo anasikilizwa na GSM kuliko wewe. Badilika Brother.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic