KOCHA mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes Da Rosa amefunguka
kuwa ushindi walioupata dhidi ya AS Vita kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya
makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ni mwanzo mzuri kwao kufanya vizuri zaidi
katika michuano hiyo mwaka huu.
Simba jana usiku iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
wenyeji wao AS Vita, katika mchezo wa kwanza wa kundi A uliofanyika katika Stade
Des Martyrs, Kinshasa nchini Congo.
Ushindi huo umeifanya Simba kuongoza msimamo wa kundi A
wakiwa na pointi zao tatu na faida ya bao moja, ambapo wanasubiri kuona matokeo
ya mchezo wa Al Ahly na Al Merrikh.
Akizungumzia furaha yao baada ya ushindi huo dhidi ya AS Vita Gomes amesema: “Tumefurahi sana na tumeridhishwa sababu tulicheza vizuri na matokeo ni mazuri.
"Kwa Simba matokeo haya yatakuwa na faida mbeleni katika hatua hii ya makundi na katika kutimiza adhima yetu ya kufanya vizuri,"
Hongereni simba hii ni kubwa si kwa simba tu bali taifa pia. Wachezaji walijituma ila benchi la ufundi mbinu zao ni kiboko.Mtu unaweza kuwa na nguvu nyingi za kulima lakini bila ya mbinu bora za kilimo kitakachotokea ni upotevu wa rasilimali nguvu.Kimbinu Didier ni bora kuliko ibenge hongera viongozi wa simba kwa umakini kwenye utafutaji wa makocha natamani wanaoisimaia Taifa stars wangekuwa na mchakato mzuri pia wa utafutaji wa makocha.
ReplyDelete