PAMOJA na kamati ya nidhamu ya Simba kutoa tamko la kumtaka Jonas Mkude kuingia kambini mara baada ya kusikiliza na kuamua juu ya tuhuma zake za utovu wa nidhamu, imebainika wazi kuwa wachezaji wenzake wamemgomea kuingia kambini hadi akose michezo 10.
Mkude alisimamishwa na uongozi wa Simba,Desemba 28,2020 kwa madai ya kuonyesha tabia ya utovu wa nidhamu, jambo ambalo lilipelekwa kamati ya nidhamu ya klabu hiyo, ambayo inaongozwa na Kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Selemani Kova, kumpiga adhabu kulipa faini ya Sh mil 1, karipio kali na kuwekwa katika kipindi cha uangalizi cha miezi sita huku ikimtaka aombe radhi.
Chanzo chetu kutoka ndani ya kambi ya Simba, kimeeleza kwamba, wachezaji wa klabu hiyo kwa jumla wamepinga kurejeshwa kambini kwa Jonas Mkude kwa madai ya kuwa hadi amalize adhabu yao waliyompa ya kuwa nje ya kikosi hadi mechi 10 zitakapomalizika.
“Mkude kwa sasa hawezi kuingia kambini kutokana na uongozi wa wachezaji kwa jumla kukataa kumruhusu kurejea hadi atakapomaliza kutumikia adhabu yao waliyompa ya kutohusika kwenye mechi 10 za timu.
"Kauli yao imeleta malalamiko kwa baadhi ya viongozi huku wengine wakijaribu kuwashawishi wachezaji ili wamruhusu kuingia mazoezini, jambo ambalo wamegomea na kuutaka uongozi kama utalazimisha basi hata wao siku wakitenda makosa wasiadhibiwe kwa namna yoyote ile kama Mkude atarejea kambini kabla ya kumaliza kutumikia adhabu yao hiyo,” kilieleza chanzo.
Tangu asimamishwe mpaka sasa Mkude amekosa mechi nane ambazo Simba wamecheza za michuano yote hivyo amebakiza michezo miwili kabla ya kurejeshwa rasmi.
Vlngozi mheshimu maamzi ya wachezaji musianze siasa Tena
ReplyDeleteWachezaji waajiriwa tu waache kujifanya wanajua Sana sheria, washindane ktk performance sio kumuwekea mwenzao kauzibe
ReplyDeleteHuyu mkude anaelekea public relationship yake ni mbovu, ajitahidi kujirekebisha vinginevyo ataviruga timu. Ukiona unakataliwa na wengi basi wewe una tatizo, fanya kujitathimini
ReplyDeleteNawapa hongera wachezaji kwa msimamo wao kwani inatokana na upendo wao usio na mipaka kwa timu yao na uongozi, lakini kwa upande wa pili, wachezaji nao waheshimuu maamuzi ya viongozi kwani hao ni kama wazee wenu wanaokupendeni na kukupeni kila aina ya heshima na kukutakieni kila la heri na matokeo yake ni namna timu ilivotulia jinsi nyote mnavopendana jambo ambalo ndio shina la mafanikio ya timu. Msameheni mwenzenu kwani samahani ni sifa kwa waungwana
ReplyDeleteNawapongeza wachezaji. Kama ni kweli huu ni mfano wa kuigwa. Wachezaji wamejiwekea misingi bora ya nidhamu. Imebaki michezo 2. Hii ndo SIMBA ya nidhamu
ReplyDeleteMkude.asipobadilika awamu hii itakua kashndikana ukiona at wachezaji wenzio wanafikia apo ujue walishakuchoka ni jambo la aibu na hatari kwa maisha yako Mkude.angalia mdogoangu utapotea
ReplyDeleteJanuary 31, nilisema..Kitakacho mwondoa Mkude Simba: "wachezaji wenzake wamemgomea kuingia kambini hadi akose michezo 10."
ReplyDeleteAkifanya mchezo Mkude nae anakaribia umri wa kuitwa babu, wajukuu watamuuliza, kweli babu eti ulikosa nidham Mpaka wachezaji wenzako wakakugomea na ikawa ndio sababu ya kupoteza mshahara wa milioni kumi na saba? Akumbuke akijikwaa tena ndio itakuwa mwisho wake na hata hao matopolo watakuogopa na marafiki kukuacha mkono kama tajiri aliefilisika na kupoteza kila alichokuwa nacho
ReplyDeleteAende tu kwao Matombo akalime mpunga
ReplyDeleteHao viongozi wanao taka mkude arudi kambini pia hawatufai pale simba,maana inaonekana hawazingatii maadili wao wanaangaliwa uswahiba unapo mpa mtu adhabu muache aimalize kama kweli unataka ajirekebishe na hiyo tabia mbovu sio leo unamuadhibu kesho unamsamehee ata siku nyingine ata kuwa haogopi adhabu zako
ReplyDeleteHao viongoz wa timu wanashida,ukiona had wachezaj wameingilia kati manake kuna mchezo mchafu unaendelea ndan ya timu
ReplyDeleteSimba wote ni wamoja na hakuna wa kutenganisha
ReplyDeletewachezaji ni waajiriwa kwenye timu iweje wamzuie mfanyakaz mwenzao?
ReplyDelete