HATIMAYE Klabu ya Liverpool imekamilisha usajili wa mabeki wawili muda mfupi kabla ya dirisha la usajili halijafungwa jana Jumatatu, Februari Mosi.
Mabeki hao wa kati ni Ozan Kabak na Ben Davies ikiwa ni lengo la kuboresha safu ya ulinzi ambayo ilikuwa inasumbuliwa na rundo la wachezaji ambao ni majeruhi ndani ya timu hiyo amayo ni watetezi wa Ligi Kuu England.
Miongoni mwa mabeki ambao ni majeruhi ni pamoja na Matip, Fabinho huku Virgil van Dijk na Joe Gomez wakiwa ni miongoni mwa mabeki wa kikosi cha kwanza na kuna hatihati wakakosekana uwanjani msimu mzima.
Kabak amejiunga na timu hiyo kwa mkopo uliogharimu pauni milioni 1.5 akitokea Klabu ya Schalke na una kipengele cha kumnunua mazima ikiwa watamhitaji kwa pauni milioni 18 pia Davies amejiunga na timu hiyo kwa dili la pauni milioni 2 akitokea Klabu ya Preston.
Jurgen Klopp amesema kuwa ana amini wachezaji hao watafanya kazi kwa ushirikiano ndani ya timu hiyo ili kupata matokeo chanya kwa kuwa wachezaji hao bado ni vijana na wana nguvu ya kufanya kazi vizuri.
"Kabak yupo vizuri na ana kipaji kikubwa na kwa Dave bado ni kijana na ana nguvu hivyo tuna amini atafanya vizuri tayari yupo ndani ya Liverpool, tunahitaji kujenga timu imara hilo lipo wazi," amesema.
xf
ReplyDelete