MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi leo Uwanja wa Mkapa kuona burudani na namna watakavyozichukua pointi tatu.
Kagera Sugar inakutana na Yanga iliyo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 19 na kukusanya pointi 45.
Yenyewe imejijengea ngome nafasi ya 10 na ina pointi 23 baada ya kucheza mechi 19.
Imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Gwambina, Uwanja wa Kaitaba kwa bao la mshambuliaji wao namba moja Mhilu Yusuph mwenye mabao matano.
Leo inakutana na kinara wa Yanga kwa utupiaji wa mabao Deus Kaseke ambaye alitupia kwenye mchezo wa mwisho walipocheza Mbeya mbele ya Mbeya City kwenye sare ya kufungana bao 1-1.
Walipokutana Uwanja wa Kaitaba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Kagera Sugar ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kuziacha pointi tatu mazima.
Akizungumza na Saleh Jembe, Maxime amesema kuwa wamejipanga kutoa burudani na kuchukua pointi tatu.
"Walikuja nyumbani wakatufunga na kuchukua pointi tatu, basi nasi tumekuja kwa Mkapa tunahitaji pointi tatu na tutatoa burudani.
"Unajua kwetu sisi ni mara chache kuingia ndani ya Uwanja wa Mkapa, sasa tumekuja nasi tunahitaji kuwafuata pale juu ambapo wapo.
"Mbinu ya kuwafikia ni moja tu kupata ushindi ndani ya uwanja na kupata pointi tatu, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti na kuona burudani," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment