UONGOZI wa Yanga umesema kuwa leo utakuwa na sherehe maalumu kwa ajili ya klabu hiyo kutimiza miaka 86.
Sherehe hiyo inatarajiwa kuanza majira ya saa 11:00 jioni kabla ya timu hiyo kumenyana na Kagera Sugar.
Ofisa Uhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Mkapa ili kushuhudia jambo lao.
Ikimaliza sherehe hiyo wachezaji watakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Kagera Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Mecky Maxime.
Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Yanga ilishinda bao 1-0 hivyo leo kazi itakuwa kubwa kwa timu zote mbili kusaka ushindi.
Mchezo wao wa ligi uliopita Yanga ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mbeya City huku Kagera Sugar ikiwa imetoka kupata sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Gwambina FC.
Hizi sherehe ndio zinaleta shida. Kazi ya nyingi ni ushindi na lengo ni ubingwa mwaka huu. Hayo mengine sherehe, kuogelea hatuyahitaji kwa sasa
ReplyDelete