February 18, 2021


 FISTON Abdol Razack ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga amekingiwa kifua na Kocha Mkuu wa timu hiyo Cedric Kaze raia wa Burundi kwa kushindwa kuonyesha makeke ndani ya uwanja.

Nyota huyo ambaye amesaini dili la miezi sita mchezo wake wa kwanza ilikuwa ni dhidi ya African Sports, Uwanja wa Azam Complex alitumia dakika 78 katika mchezo wa kirafiki na mchezo wake wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara ilikuwa dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine.

Kwenye mchezo huo wakati Mbeya ikipata sare ya kufungana bao 1-1 nyota huyo alitumia dakika 74 na nafasi yake ilichukuliwa na Ditram Nchimbi, alishindwa kuonyesha makeke ambayo mashabiki wake walikuwa wanahitaji.

Kaze amesema kuwa bado hajajenga mazoea mazuri na wachezaji wenzake ndani ya uwanja hivyo atakuwa kwenye ubora wake kwenye mechi zake zijazo, mashabiki wasiwe na mashaka.

“Ni mchezaji mpya kwa sasa bado hajazoea ile mikimbio ya wachezaji wenzake kama ambayo naye hajawazoea, ila nina imani kwamba baada ya muda atakuwa kwenye ubora na atafanya vizuri ndani ya uwanja,” amesema.

Jana, Februari 17, Yanga ilikamilisha kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Kagera Sugar inayonolewa na Mecky Maxime Uwanja wa Mkapa na kwenye mchezo wa kwanza msimu huu, Yanga ilishinda bao 1-0, Uwanja wa Kaitaba.

Mchezo wa jana waligawana pointi mojamoja kwa kufungana mabao 3-3, mchezo ambao umekusanya mabao mengi ndani ya uwanja wa Mkapa kwa msimu wa 2020/21.

Kwenye mchezo huo Fiston hakuwa sehemu ya kikosi hicho cha Yanga inayoongoza ligi ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 46 baada ya kucheza jumla ya mechi 20.

3 COMMENTS:

  1. Sisi wenyewe tunawaharibu wachezaji kwa namna tunavyowapamba wakati wa kuwasajili na kuwapokea. Tunawaaminisha kuwa wao wako juu sana kiasi kwamba hawana ushindani hapa bongo
    Tatizo linaanza pale anapokuta kumbe wavumao papa kumbe wako wengi.

    ReplyDelete
  2. Tatizo la sasa la Yanga lipo kwa Kocha Kaze, Kaze anawalinda sana baadhi ya Mastaa ambao viwango vyao vimechusha, anachelewa sana kufanya sub inapobidi na ni mbishi/hataki kukosolewa.
    Ndo maana hakumpenda Mwambusi. Mecho za Mbeya City na Kagera zimethibitisha hili, baada ya sub zilizo chelewa timu ilibadilika.
    Kaze hawezi kupata msaada stahiki kutoka kwa Nizar Halfan hasa ligi inapoelekea magharibi.
    Wazungu husema "dont disturb an operating system"...usiubugudhi mfumo unaofanyakazi vizuri. Ile timu iliyomalizia mzungo wa kwanza ipo wapi?
    Kwa nini defence ya Yanga ni nzito na inakatika sana?

    ReplyDelete
  3. Sisi mashabiki tunaumia paleambapo hatupati matokeo mazur jaman huu ubigwa mbona twaupoteza wakati tulianza vizuri? Kocha tunakuamini ndomana tukakuleta jangwan turudishie heshima yetu wananch

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic