February 21, 2021


 MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze amesema kuwa kinachombeba ndani ya kikosi hicho ni juhudi pamoja na ibada.

Ikiwa ipo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 21 na imefunga mabao 34 amehusika kwenye mabao nane akiwa amefunga mabao sita na kutoa jumla ya pasi mbili na ni kinara wa utupiaji ndani ya kikosi hicho.

Alianza pia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara jana wakati wakishinda bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Mkapa.

Kaseke amesema:”Kikubwa ni juhudi pamoja na kumuomba Mungu ambaye ni muweza wa yote, hivyo bado tunazidi kupambana mashabiki watupe sapoti tutafanya vizuri,”.

Yanga inaongoza ligi ikiwa imekusanya jumla ya pointi 49 inafuatiwa na watani zao wa jadi Simba ambao wapo nafasi ya pili na pointi zao ni 42 baada ya kucheza mechi 18.

4 COMMENTS:

  1. Kaseke nae kawa mtambo wa wabao, duh! Huyu ni mtambo wa ulozi tuu hana lolote zaidi ya hilo. Mbeba mikoba wa timu huyo.

    ReplyDelete
  2. Kweli ushindi ulevi hako kabao ka uganga ka karinyos ndio pov u linawatoka hahaha

    ReplyDelete
  3. Haya ni masihala kabsa kwa mfumo huu wa Gori 6 et ndio mtambo wa yanga hivi mfungaji Bora tutatoa kwer?🤔

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic