February 22, 2021

 

NAHODHA wa Al Ahly, Aiman Ashraf amesema kuwa wamekuja Dar kwa ajili ya kupata ushindi mbele ya wapinzani wao Simba.

Kesho, Februari 23 Al Ahly itakaribishwa na Simba, saa 10:00 kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya makundi.

Mchezo huo unatarajiwa kuchukua jumla ya mashabiki 30,000 kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Afrika,(Caf) kwa ajili ya kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

Nahodha huyo amesema:"Lengo letu kubwa ni kutwaa ubingwa na tunajua tunacheza na timu kubwa hivyo hatutadharau jambo lolote.

"Kuhusu muda wa mechi hauwezi kuwa kikwazo kwetu. Tumekuja kupambana tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo hivyo tutaingia kwa tahadhari na tunawaheshimu wapinzani,".

3 COMMENTS:

  1. Wajue hii siyo Simba ya Ucheba waliyoifunga mabao marano ugenini kwani ni Simba iliyonona kila upande

    ReplyDelete
    Replies
    1. AKIMALIZA DAKIKA 45 TU ZA AWALI ATAWAAMBIA WENZAKE KWAMBA JAMANI HAPA TUTAFUTE SARE NA SIO USHINDI

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic