February 14, 2021


 KOCHA Mkuu wa Klabu ya Namungo, Hemed Morocco amesema kuwa mambo ambayo wamekutana nayo nchini Angola ni sehemu ya mchezo jambo ambalo linawafanya wajipange kwa ajili ya wakati ujao.

Namungo Februari 12 ilisafiri kutoka Bongo mpaka Angola kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora dhidi ya 1 de Agosto ya Angola.

Kilizuiwa Uwanja wa Ndenge wa Luanda Februari 13 kwa kile ambacho kilielezwa kuwa wachezaji wao watatu pamoja na kiongozi mmoja kukutwa na Virusi vya Corona.

Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) pamoja na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya nje waliweka nguvu kwenye kufuatilia suala hilo ambapo majibu yalitolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwamba mchezo wao ambao ulipaswa kuchezwa leo umefutwa na Kamati ya maadili italifuatilia suala hilo kwa ukaribu.

Kikosi cha  Namungo kinatarajiwa kurejea leo Februari 14 baada ya mchezo huo kufutwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Morocco amesema kuwa wanashukuru Mungu wapo salama ila yaliyotokea ni somo kwao.

 "Ni changamoto kwetu na ni somo pia hivyo hatuna la kusema kwa sasa,tunarejea kujipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo" ..

11 COMMENTS:

  1. Msichukulie poa, Suala la Corona bado ni tatizo kwa nchi nyingi, kama watu walienda bila kupima ndio wajifunze next time wachukue vipimo, watu wako serious na suala la Corona

    ReplyDelete
  2. Namungo waache uswahili, next time wawahi kufika kituoni siku 4 -5 kabla na watangulize watu, ligi za CAF zina pesa; siyo lelemama

    ReplyDelete
  3. Mmesoma maelezo vizuri? Kweli Korona ipo, ila wamesema wachezaji watatu na kiongozi mmoja ndio walikuwa na korona, sasa kwa nini wasingewazuia hao na wakaacha wengine wacheze mechi. Hao jamaa wakuda.

    ReplyDelete
  4. Walikuwa wanataka timu nzima ikae karantini

    ReplyDelete
  5. woga tu wa watu wa Angola hawataki kushindwa mechi, kwani vipimo vya TZ na huko ni tofauti au wanatumia kile kipya������

    ReplyDelete
  6. Hawa Waangola wamebugi kama ni watu wanne waligundulika kuwa na maambhkizi ya Corona. Je kwa nini timu nzima ilipelekwa nje ya mji tena chini ya ulinzi wa jeshi. Nawaza kwa sauti na kwa akili ya kawaida tu nawaona de Agosto kama wamejiondoa wenyewe kwenye mashindano vile, na mbaya zaidi waliyafanya hayo mafigisu yote bila kuwasiliana na CAF, ndo maana kamati ya maadili ya CAF inalichunguza sakata zima

    ReplyDelete
  7. Hakuna anayebisha kuwa Corona ipo hata CAF wanalijua hilo ndo maana wametoa miongozo mbalimbali. Waangola wamefanya figisu za kishamba kutaka kuiweka timu nzima karantini. Kwa akili ya kawaida wanamaanisha kuwa Angola si salama kwa soka. Kwa mantiki hiyo wao wakae kando wawaache wengine wasonge huku wakichukua tahadhari.

    ReplyDelete
  8. Suala la Corona ni tete. Kuna baadhi bado hamna uelewa nalo. Kama ni kweli kulipatikana kesi ya Corona hama angelikuwa mtu mmoja katika msafara ilitosha wote kukaa karantini. Wengi mmesikia jinsi wacheza tennis walivyowekwa karantini Australia baada ya mtu mmoja kupatika na Corona katika ndege waliyopanda. Mashindano yaliahirishwa na ukawa mjadala wa kitaifa. wachezaji walikuwa wanafanya mazoezi vyumbani hotelini

    ReplyDelete
  9. Msiongee mambo msiyoyajua kuhusu corona,kwenye Kundu loloye la watu waliokusanyika pamoja au kusafiri pamoja ,anapogundulika mmoja wenu ana covid 19 basic inapaswa Kundu Zima likae karantini kwa Muda usiopungua siku Kumi Hadi Kumi Na Tano,kwa hiyo waangola walikuwa sahihi kabisa,kama ushamba tunaosisi watanzania ambao tunajiona tunajua sana kumbe tunaungua Na jua,watanzania hatuwafikii waangola kimaendeleo ya nchi mpaka ya watu wake tembeeni mjionee msingoje kuambiwa

    ReplyDelete
  10. Samahani niliteleza kidogo kiuandishi niliandika Kundu badala ya kundi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic