February 19, 2021


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hautendewi haki kwenye masuala yao tofauti na wengine namna ambavyo wanafanyiwa ikiwa ni pamoja na sakata la mchezaji wao Bernard Morrison ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya Simba.

Morrison amekuwa na mvutano mkubwa na mabosi wake hao wa zamani ambapo wao wanadai kwamba ana kandarasi ya miaka miwili ndani ya Yanga huku mchezaji akiweka wazi kuwa alisaini dili la miezi sita. 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredric Mwakalebela mwishoni mwa 2020 aliweka wazi kuwa mchezaji huyo alisaini mkataba feki jambo ambalo limefumbiwa macho na wahusika pamoja.

Pia amesema kuwa Morrison alitakiwa kulipa fedha kwa kwa Yanga ila mpaka sasa imekuwa kimya tofauti na wao wanapofanya makosa kupewa adhabu mara moja.

Mwakalebela amesema:"Mkataba feki wa mchezaji mpaka sasa imekuwa kimya, tunaomba tuitwe tuthibitishe, ukweli kuhusu suala hilo ila tunamaliza ligi hatujaitwa.

"Kamati ilisema mchezaji anapaswa arudishe fedha kwenye Klabu ya Yanga, hadi leo hakuna suala hilo kuona linazungumzwa na hakuna majibu na hakuna suala linalozungumziwa.

"Hatujasikia TFF,(Shirikisho la Soka Tanzania) likisema kuwa mchezaji huyo amelipa ama kuna taarifa yoyote inayohusu malipo yake.

"Ila ikitokea sasa ni suala la Yanga limetokea muda huohuo adhabu inatolewa kwa wakati na utaskia tunaambiwa kwamba tunakatwa kwenye mapato ya getini," .

11 COMMENTS:

  1. Wamshamlipa Tambwe na wengine wanaowadai tuanzie hapo kwanza

    ReplyDelete
  2. Hili swala la Morrison si limepelekwa CAS/FIFA kwa mujibu wa Mwakalebela.Sasa TFF achukue uamuzi gani ikiwa Yanga amekata rufaa dhidi ya TFF?Kanuni za bodi ya ligi ziko wazi kwa mashabiki wa timu wakifanya fujo, refa kutozingatia sheria za uchezeshaji anapewa adhabu.Viongozi hamtaki kupeana adhabu kama mashabiki wenu wanaleta fujo uwanjani??Kama Yanga wanaona wanaonewa wao tu basi jitoeni ktk ligi ya VPL na mkajiunge na ligi ya zanzibar.

    ReplyDelete
  3. Mambo yamebadilika kutoka Morisson ni mchezaji wetu mpaka tulipwe fedha zetu zilizoamuliwa na kamati ya maadili.
    Vipi hadithi za CAS vipi tena?
    Manara aombe radhi kwa kosa gani?
    Wao waitanie Simba wakitaniwa iwe nongwa.
    Kweli safari hii Utopolo wamepata viongozi feki haswa.
    Presha ya ligi imewashinda wanaanza kutafuta visingizio.

    ReplyDelete
  4. Haya ndio yanayowaumiza Yanga. Badala ya kujishughulisha na timu muikwambuwa kutokana na mwendi kuchechemea. Inaonesha jamaa wana shida ya pesa wanasema hawajalipwa hela yoyote, wamesahau kuwa Tambwe mleopewa muda wa kumlipa haki yake bado hamjafanya hivo au ndio mnazingojea za Morrisson ndio mumlipe? Inaona kwa jamaa mambo yatokota chini kwa chini na letu ni jicho tu

    ReplyDelete
  5. Kila Morisson akifunga Utopolo wanaanza kesi upya. Ila sasa wamebadili mwelekeo. SIO mchezaji wao vali walipwe pesa walizompa Morisson!Walimpa pesa za nini wakati dio mchezaji wao na mkataba wa miezi 6 uliisha??

    ReplyDelete
  6. Utopolo bwana wana kichaa...Kila Morrison akifunga goli wanakerwa na kuanza longo longo..Yule ni mfungaji..na atafunga magoli saana... Bora umeweka picha yake akiwa katika jezi ya Yanga..labda roho yao itatulia

    ReplyDelete
  7. Mwakalebela anashindwa kujibu hoja za msingi,matatizo ya Timu yetu kutofanya vizuri na status ya kesi CAS,Zipo taarifa kesi haisikilizwi mwaka huu atuambie.Tumechoka kila timu ikifanya vibaya unaibuka na hoja za kijinga kutupoteza maboya.Rudi kwenye siasa hutufai Yanga

    ReplyDelete
  8. Ni dhahiri kuwa Yanga sasa inashida ya pesa na muda waliopewa unatiweka kwa kasi na Tambwe hajalpwa na bora hilo waliweke wazi ili bakuli lianze kazi yake upya.

    ReplyDelete
  9. Kweli maneno yako. Kila Morrisson anapotia goli wao huabza hucharuka apya na sasa hawapati usingizi kila wakififkiria siku watapopambana na Mnyama na Morrisson yumo ndani na itapotekea Morrisson kuuwacha mbili ndio hapa baada ya mechi mojakwamoja Mpaka TFF wanamtaka Morri au walipwe hela HAHAHAAA

    ReplyDelete
  10. Mwakalebela Wacha kutufanya wajinga.Manara katutania kama sisi tunavyowatania mikia.
    Usitafute mchawi tuelezeni kwanini timu haifanyi vizuri.
    Kusingizia kwamba eti jezi zimedorora kwa sababu ya utani wa Manara ni kutufanya wajinga wanayanga.

    ReplyDelete
  11. Tumechoka sasa na mambo ya kitoto yanayofanywa na Utopolo SC. Inaelekea Morrison anawakera sana hasa kila anapocheka na nyavu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic