DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kwenye mchezo wao dhidi ya Biashara United atawafuata kwa tahadhari na atwatumia wachezaji wake wote kusaka ushindi ndani ya uwanja.
Simba imetoka kumalizana na AS Vita kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi na ilishinda bao 1-0 na kuifanya ikisanye pointi tatu ugenini.
Ipo nafasi ya pili kwenye msimamo kwa tofauti ya mabao ya kufunga, imefunga bao moja huku vinara wa kundi hilo ambao ni Al Ahly wakiwa na mabao matatu.
Februari 18 Simba itakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Karume, Mara.
Kikosi kipo Mwanza ambapo leo kitaanza safari kuelekea Mara kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Gomes amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu ila wapo tayari kupata pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.
“Tunatambua kwamba mchezo wetu utakuwa mgumu ila tutapambana kupata pointi tatu muhimu ndani ya uwanja, kila kitu kipo sawa na wachezaji wote watatumika kusaka ushindi kwa kuwa wapo vizuri,” amesema.
Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 39 baada ya kucheza jumla ya mechi 17, imekusanya pointi 39.
Inakutana na Biashara United iliyo nafasi ya nne na pointi zake ni 32 baada ya kucheza jumla ya mechi 19.
Walipokutana Uwanja wa Mkapa, Simba ilishinda mabao 4-0 hivyo mchezo huo utakuwa ni kisasi kwa Bashara United inayonolewa na Francis Baraza.
Baraza amesema kuwa wanatamua utakuwa mchezo mgumu ila wapo vizuri na wanahitaji pointi tatu.
Mchezo wa leo uwe wakujima kuikabili Al Ahli ambayo ni timu ngumu kuliko zote Africa. Si tuliiona jana namna ilivoielemea Al Marikh
ReplyDelete