February 17, 2021

 


MWAMUZI  Ludovic Charles ambaye alichezesha mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Mbeya City na Yanga, Uwanja wa Sokoine kwenye sare ya kufungana bao 1-1 jina lake ni miongoni mwa waamuzi ambao watajadiliwa na Kamati ya Waamuzi hivi karibuni ili kuweza kufanya tathimini ya kile ambacho alikifanya.

Mwamuzi huyo alionekana kulalamikiwa na wachezaji wa timu zote mbili kwa kuyakubali mabao mawili ambayo yalikuwa na utata na baada ya kumaliza mchezo wachezaji wa Yanga walionekana kumfuata tena jambo lililofanya atoke chini ya ulinzi huku nahodha Lamine Moro akiwatuliza wachezaji wake.

Miongoni mwa mambo ambayo yalionekana kulalamikiwa ndani ya Uwanja wa Sokoine ni pamoja na tukio la fair play dakika ya 25, Mbeya City walikuwa kwenye umiliki wa mpira ila mwamuzi alisimamisha mpira kwa kile alichodai kuwa kuna mchezaji wa Yanga amechezewa faulo.

 Dakika ya 67  Deus Kaseke baada ya kuingia akichukua nafasi ya Farid Mussa aliweza kubadili mchezo na Kaseke alionekana kuchezewa faulo ndani ya 18  dakika ya 77 na mchezaji wa Mbeya City.

Tukio hilo mwamuzi alipeta na kuruhusu Mbeya City waendelee na mchezo ndani ya Uwanja wa Sokoine jambo ambalo lililamikiwa na wachezaji.

Bao la Kaseke wa Yanga, alifunga dakika ya 84 na lilionekana kuwa na utata kwa kuwa mchezaji mmoja wa Mbeya City alionekana akiokoa mpira ule kabla ya kuvuka mstari.Tukio hilo lilisababisha wachezaji wa Mbeya City kumlalamikia na kipa namba moja Haroun Mandanda alionyeshwa kadi ya njano.

Penalti ya Yanga iliyotolewa na Lodovic dakika ya 90 baada ya Yassin Mustapha kufuatwa na mpira wakati akiruka ndani ya 18 ililalamikiwa na wachezaji wa Yanga na ilisababisha kadi ya njano kwa nahodha Lamine Moro.Penalti hiyo ilifungwa na Pastory Athanas.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Tanzania, Sud Abdi Mohammed alisema kuwa hawezi kuzungumzia maamuzi ya kwenye mchezo huo wa Mbeya City na Yanga kwa kuwa ipo kamati inayoshughulikia makosa.

“Ukitaka nizungumzie maamuzi ya mchezo wa Mbeya City na Yanga huo kwa sasa sitaweza kuzungumzia kwa kuwa  ipo kamati maalumu ambayo huwa inakaa kujadili masuala yanayohusu maamuzi.

“Ikiwa nitasema nizungumzie jambo hilo ninaweza kuonekana ninamtetea ama kumkandamiza hivyo hilo tuachie kamati itafanya kazi yake.

“Ila kabla ya mzunguko wa pili kuanza tulitoa mafunzo ya vitendo na nadharia kwa muda wa siku tano ambapo tulianza Januari 29 mpaka Februari 2  kwa waamuzi wa Ligi Kuu na tuliwapeleka uwanjani na darasani na tuliwaambia wazingatie sheria na kuchezesha kwa umakini,” amesema.

Cedric Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa alishangazwa na maamuzi wa mchezo huo jambo ambalo hakulitarajia.

Mathias Lule, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa kuhusu mwamuzi kuamua bao lile hana cha kufanya kwa kuwa hawezi kubadilisha maamuzi yake.

 

18 COMMENTS:

  1. Mbona mashtaka kama hayo hata mara moja hatuyasikii kwa Mnyama Hata pindi yanapotokea dhidi yake? Haya yote kwa Yanga yanasabsbishwa na panic kubwa waliokuwa nayo ya kukosa magoli droo nyingi na kuohopa kuukosa ubingwa baada ya majitayarisho na gharama kubwa sana ambayo hazijawahi kutokea

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uya sikii kwa simba kwasababu kazi yako ni kushoboka mambo ya yanga

      Delete
    2. Suala la ghalama ambazo young Africans wametumia haihuxiani kabxa na maamuzi ya uwanjani xuala la ghalama ni jukumu la timu na kama timu imelitekeleza hilo baxi na waamuzi watekeleze jukumulao la uamuzi bola kama inavyotakiwa

      Delete
  2. Tunapanda ngazi halafu halau twarudi chini

    ReplyDelete
  3. Mwaamuzi yeyote hata atoke EPL akikubali kuchezesha mechi ya yanga dhidi ya timu yoyote hata iwe yanga princess ajiandae kupelekwa kamati ya waamuzi maana hawa jamaa sio kwa gubu hili walilonalo. Wanapresha ya kupata ubingwa bila hata kuangalia uwezo wao na wa timu zingine. Tatizo lilianzia pale walipobuni mtindo wa kununua waandishi na wachambuzi uchwara kuwajaza matumaini hewa mashabiki wao.

    ReplyDelete
  4. Mpira ulimfuata mchezaji hii ni kali kuliko zote kuwahi kusikia nadhani ipo siku mpira utakimbia mchezaji asiupige

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi wana msulubu refarii kwa kosa lipi hasa?Wewe mwandishi ulisoma kozi ya urefarii?90% ya wachambuzi na marefa veterani wanasema ukisha nyanyua mikono juu na mpira ukigonga huo mkono ni faulo pasipo shaka.Rejea video clip ya Simba vs Vita uangalie scenario ya mchezaji wa Vita aliyenawa mpira na kuamuliwa penalti ambayo mazingara hayo hakuna tofauti na ya Mustafa Yasin.Ni penalti pasipo shaka.Kama kuna timu zinafikia hiatua ya kulalamikia marefarii basi ni bora wakaanzisha ligi yao na marefarii wao au wajiunge na ligi ya Zanzibar.

      Delete
  5. Yule wa simba na yanga alitoa penati ya nje ya 18 pamoja na kuwepo waamuzi 6 na kuinyima simba penati za wazi hawajamjadili hadi leo waache double standard

    ReplyDelete
  6. Hahahahahaaa, nianze kwa kucheka kwanza, nchi ya Tanzania kila kitu magumashi na ndio maana hatupigi hatua katika soka letu longo longo kila kukicha ratiba za mechi hubadilishwa kila siku marefa kuwekwa kiti moto kila siku na ndiomaana hatutoi marefa kimataifa, na wewe mtani wangu taratibu bwana naona kwa vile uko vizuri basi unatukebeeehi hahahaaaa ila wewe ndio mtu wa ajabu sana unachanganya maji na mafuta ukipoteza game tu basi unakimbilia POLISI we uliona wapi hiyo mtani mambo ya mpira wa miguu uyapeleke POLISI eee mtani hahahahaaaaaa hiyo ndio TANZANIA bwana

    ReplyDelete
  7. Acha ushamba kwani Yanga ndo wanawapeleka waamuzi kwenye kamati. Sema mashitaka yanayoihusu Simba kama inakula kwao lazima TFF iyafiche isitoe matokeo kama mlezi wa madhambi yao

    ReplyDelete
  8. Bado sana soka letu Tz lina maajabu sana. Kuna timu mbeleko hapa inashinda kiajabu ajabu lakini kamati hazikai. Na hizi kamati ni ovyo kabisa, adhabu eti amefungiwa miezi sita, then anarudi tena kuja kuboronga. Kufungiwa kunasaidia nini wakati timu ishanyimwa ushindi. Inabidi anayeboronga kwa makusudi afutiwe leseni kabisa na kutojihusisha na soka maisha.

    ReplyDelete
  9. Ungeandika kutokana na bao la utata la yanga sio mabao yenye utata

    ReplyDelete
  10. Ungeandika kutokana na bao la utata la yanga sio mabao yenye utata

    ReplyDelete
  11. ile sheria ya mpira kuufuata mkono ilibadilishwa,sasa ni kwa namn ayoyote ukigusa mkono unapewa adhabu, isipokuwa kwa hekima za mwamuzi. Yang an aSimba huwa zinabebwa sana sana kwahiyo mwamuzi kiw afair tu lzima alaumiwe! Game ya Yanga na KMC Mwanza, mwamuzi aliibeba Yanga wazi, mechi ya Simba na KMC Eli Sasii alipewa malekezo kabisa kuwa Simba ishinde kwakuw aina mchezowa kimataif mbele ili wachezaji wawe na ari.TFF msidhanihatufahamu haya. Mnaharibu mpira. Ndio maana hakuchukuliw ahatua yoyote. Mchezo wa robo final ya Azam Federations iluyopit akatiya Yanga na Kagera, mwamuzi alipewa maelekezo ili Yanga ipite, aliboronga ammmno lengo ilikuwa Yang ikutane na Simba nusu final. Mlifanikisha HILO TFF. Ndiyo maana hakuadhibiwa. This is non sense.

    ReplyDelete
  12. Inasikitisha saana kuona kadri siku zinavyozidi kwenda badala ya soka letu kwenda mbele ndokwanza linazd rudi nyuma kutokana na maamuzi yaajabu yanayofanywa na waamuzi kila kukicha kisingzio eti nao ni binaadam ......inasikitisha sana kila nkiiangalia future ya soka letu mpaka YESU aludi nahx ndiotutaendlea kisoka 😒☹😟

    ReplyDelete
  13. Mpira sikuhizi unamacho unafuata mkono sheria ya ukabaji ndani ya 18 tunaijua au makelele mengi ukae torongaga kuleka kikizile kokung'una inguo lazima tutafakari mpira ni mchezo wa uwanjani uko wazi kama timu yako haichezi vizuri bas sema tuache nonsens propaganda

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic