ANTHONY Martial, amejikuta akiingia katika wakati mgumu kwa mara nyingine baada ya kushambuliwa mitandaoni wakati timu yake ya Manchester United ikipata sare ya bao 1-1 dhidi ya West Bromwich Albion, Jumapili.
Mfaransa huyo alianza katika kikosi cha kwanza kabla ya kutolewa dakika ya 66 baada ya timu yake kushindwa kuonesha makali ya kufunga ili kuwafukuzia kwa ukaribu wapinzani wao, Man City ambao wanaongoza katika msimamo wa Premier League.
Mara baada ya mechi hiyo kumalizika, kulianza kusambaa meseji za ujumbe wa chuki na nyingine za ubaguzi wa rangi zikiwa na alama au picha mbalimbali zinazoonesha ubaguzi kupitia Mtandao wa Instagram.
Hii ni mara ya pili kwa mshambuliaji huyo kushambuliwa hivi karibuni tangu kuanza kwa mwaka huu, mara ya kwanza ilikuwa baada ya United kufungwa 2-1 na Sheffield United.
Wachezaji wengine wa Premier League ambao wamewahi kuhusika katika kushambuliwa kwa maneno kama ilivyo kwa Martial ni Reece James na Antonio Rudiger wa Chelsea na Romaine Sawyers wa West Brom.
Kumekuwa na presha nyingi juu ya watu wanaohusika kutoa kauli za kibaguzi mitandaoni, wadau wa soka wakiwemo wachezaji wakitaka mitandao husika iwafichue na ikiwezekana iwafungie lakini haijawa hivyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment