February 17, 2021


MFUNGAJI wa bao pekee la Simba katika ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita, Mkongomani, Chris Mugalu,ameibuka na kutamba kuwa lazima kitaeleweka msimu huu katika michuano hiyo inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Mkongomani huyo bao lake la penalti dakika ya

60, lilitosha kuipa ushindi Simba ugenini katika mchezo uliochezwa Ijumaa iliyopita nchini DR

Congo ukiwa ni wa Kundi A.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mugalu alisema,malengo waliyojiwekea katika michuano hiyo ni kuhakikisha wanashinda michezo yote kwa kuanzia ugenini hadi nyumbani.

Mugalu alisema kuwa kikubwa wanahitaji pointi zote 18 katika michezo sita watakayoicheza ya hatua hiyo, nyumbani na ugenini katika Kundi A, lenye timu za Al Ahly, El Merrikh na AS Vita.

Aliongeza kuwa, kikubwa wamedhamiria kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya msimu uliopita kushindwa kufika huko.

“Bado tuna kibarua kigumu kiukweli katika kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hii,kikubwa tunachotakiwa ni kujipanga ili kutimiza malengo yetu.

“Siyo kazi rahisi kwetu, lakini kwa malengo tuliyoyapanga msimu huu ni kuhakikisha tunashinda michezo yote ya ugenini kama tulivyoanza dhidi ya Vita.

“Kama tukipata matokeo mazuri ya ugenini,ninaamini nyumbani tutakuwa na kazi rahisi kwa kuutumia vema uwanja wetu wa nyumbani,” alisema Mugalu.


SOURCE: SPOTI XTRA

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic