February 21, 2021




 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hautambui chochote kuhusu Klabu ya Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kuwa na mchezo dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Simba itashuka Februari 23 kumenyana na Al Ahy ya Misri mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya makundi na utachezwa Uwanja wa Mkapa.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa hatambui jambo lolote kuhusu Simba kuwa na mchezo mpaka pale atakapofuatilia na kujifunza.

"Kuhusu Simba kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na kuwa na mchezo sijafuatilia na bado sijajua hivyo mpaka pale nitakapojua namna walivyojiandaa pamoja na timu ambayo watacheza nayo. 

"Kwa kweli sijafuatilia kujua kwamba ni timu gani inacheza, hivyo kwa kuwa nimekumbushwa kuhusu Simba nitafuatilia.

"Katika hilo nipo kimya kwa kuwa sijui jambo lolote ambalo linaendelea.Kuhusu wao ninasema kwamba mashabiki wetu wa Yanga watupe sapoti ili tuendelee kupambana tunakwenda Tanga, tunakwenda Kilimanjaro tunakwenda kwenye Kombe la Shirikisho tuungane tukapambane.

"Nimejitoa kwa ajili ya timu yangu ya Yanga hivyo kuhusu timu nyingine siwezi kuifuatilia kwa kweli," amesema.

Kwenye msimamo Yanga ipo nafasi ya kwanza na imekusanya pointi 49.

11 COMMENTS:

  1. Maskini weweee! Watani poleni maana hakuna kiongozi hapo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwakalibela alishakuwa mpaka katibu mkuu wa shirikisho la mpira Tanzania TFF.Hapo ndipo unapopata jibu kwanini mpira wetu upo kiujinga ujinga hadi hii leo kutokana na kuwaruhusu watu wajinga kama hawa kuongoza soka letu.Na ndio maana Yanga leo kila kitu kinachotendeka wanahisi wanaonewa kwa sababu walizoea kubebwa wakati wa uongozi wa Malinzi na kina Mwakalibela. Kama kiongozi anadaganganya mchana kweupe kuwa hajui kuwa simba itacheza na Ahly vipi atashindwa kufanya udanganjifu kwenye mikataba ya wachezaji? Na ndio maana Mwakalibela ameendelea kuwadanganya wanayanga kwa mafanikio kuhusu suala la Morrison huku simba wakijibweda kwa faida ya uongo wake.Na ndio maana Yanga ipo hatarini kushushwa daraja na FIFA kwa kuwa Yanga ndio timu inaongoza east Africa kwa malalamiko ya wachezaji na makocha kutokulipwa stahiki zao baada ya kuitumikia timu hiyo.Matatizo yote hayo yanawapata yanga kutokana na kuwa na viongozi wa hovyo kama akina Mwakalibela. Tuitabirie majanga zaidi Yanga chini uongozi walionao sasa. Wahenga wamenena muombea chumvi huombea chungu chake kwa maana rahisi yakwamba ukiishi kwa chuki utarejeshewa chuki nakuhisi unachukiwa na ukiishi kwa upendo basi utarejeshewa upendo nakuhisi unaishi kwa amani na utulivu na ujinga kamwe haujengi

      Delete
    2. Na nadhani kama kiongozi mkuu wa timu ya Yanga au simba huwezi kumtofautitisha na kiongozi wa kitaifa kwanini serikali au TFF haijatoa tamko la kumtaka Mwakalibela kunyoosha sentesi zake kwenye hill? Maana kwa tafsiri rahisi hapa Mwakalibela anahamasisha chuki katika kipindi ambacho vijana wa Yanga wanahitaji maneno ya hekima zaidi ya kuwatuliza la sivyo huko tuendako ni hatari kwa afya ya usalama kwenye mpira wetu.

      Delete
  2. Ni maneno ya kiajabu kutoka kwa kiongozi wa timu kubwa

    ReplyDelete
  3. Mafuta yakizidi yanaathiri ubongo na uwezo wa kufikiri kwani damu inakuwa haisafirishwi vizuri kupitia mishipa ya damu.Hali hiyo inafanya ubongo ukose oxygen ya kutosha.
    Msimshangae kwani kwa kutambua hilo Yanga wamempa kazi chafu zote ili kukwepa lawama.
    Uliona wapi akitambulisha mchezaji au kusemea sera ya klabu?

    ReplyDelete
  4. Huo sasa ni uongo. Kweli hajui kabisa kama kuna timu zimekuja hapa kumenyana na simba na namungo? Wakati mwingine unakubali tuu hali ila unasema hayanihusu, inatosha sio kusema hajui kuwa al ahly wapo hapa nchini, huyo atakuwa sio mwanamichezo. By the way hakuenda kuwapokea al ahly this time?

    ReplyDelete
  5. Huyu amevamia tu mwenye soka Ni mchafuzi furani

    ReplyDelete
  6. ANAZEEKA VIBAYA, ALAFU SI UNAJUA ALISEMA ATAJITOA NA TIMU YAKE KATIKA LIGI

    ReplyDelete
  7. Ni aibu kwa kiongozi wa timu kubwa kuwa na wivu wa kijinga kiasi hicho yani anakuwa hana tofauti na shabiki ambaye hajitambui.... Kweli hiyo timu yake imepata hasara na sidhan kama hata hiyo timu anayoiongoza inaweza kupaata maendeleo kwa uongozi wa aina yake. Muda utaongea, ila akiendelea kuingoza kwa muda mrefu wasitegemee maendeleo yoyote

    ReplyDelete
  8. Kiongozi kama huyo hawez kufanya tathmini na kujua timu yake inakwama wapi na warekebishe wapi ila anachoweza ni kutoa maelezo ya kishabiki yasiyo na tija na kuiacha timu kuendelea kudorora na kuishia kulaumu wasiohusika

    ReplyDelete
  9. Duh! Afadhali angekuwa shabiki wa kawaida tu, Kiongozi Tena was timu kubwa kama &topolo...no. Pls

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic