February 14, 2021

 


CEDRIC Kaze,Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa malengo yao ya kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Bara yapo palepale,licha ya uwepo wa watu ambao wanawakatisha tamaa.

Jana, Februari 13 Yanga ikiwa Uwanja wa Sokoine Mbeya, ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mbeya City na kugawana pointi mojamoja. 

Yanga ilianza kupachika bao la kuongoza kupitia kwa Deus Kaseke ambaye akitokea benchi kipindi cha pili akichukua nafasi ya Farid Mussa kwa bao ambalo lilikuwa na utata dakika ya 84.

Bao hilo lilifungwa huku alionekana kwamba mchezaji wa Mbeya City aliokoa kabla mpira haujavuka mstari huku lile la Mbeya City likifungwa kwa penalti na Athanas Pastory dakika ya 90+1.

Kaze amesema:"Kuna watu ambao wanatulatisha tamaa kuelekea safari yetu ya kusaka ubingwa ila hatujakata tamaa tutaendelea kupambana.


"Wachezaji wanajituma na juhudi inaonekana hivyo wakati ujao tutafanya vizuri zaidi,mashabiki watupe sapoti bila kuchoka,".

Sare ya Yanga inawafanya wafikishe jumla ya pointi 45 wakiwa nafasi ya kwanza. Fiston Abdulazack ingizo jipya ndani ya Yanga alianza jana kwa mara ya Kwanza kutumika ndani ya Ligi Kuu Bara. 

11 COMMENTS:

  1. Hajasema ni watu gani hao wanaowakatisha tamaa. Ligi ni ngumu ajipange

    ReplyDelete
  2. Si muda mrefu tutaaikia visingizio vingi, ngoja wenye uongozi wao wqrudi kileleni

    ReplyDelete
  3. Huyu kocha ana maneno mengi mno, afanye kazi aache porojo la sivyo mbio za ubingwa ataziaga mapema maana Simba ya sasa ipo kikazi zaidi

    ReplyDelete
  4. Mzee wa muunganiko kaanza visingizio... Sasa ndio ataijua ligi ya bongo sio lelemama. Ajipange kwa fitna za ndani na nje ya uwanja. Waache kuwekeza nje ya uwanja wataliaa... 🏃‍♂️🏃‍♂️🚴‍♂️

    ReplyDelete
  5. Ivo bado wanataraji kupata ubingwa. Inafaa afanye hivo kwasababu kwa matokeo ya Timu yalivo, anajijuwa kakalia tawi kavu

    ReplyDelete
  6. Wamejipanga kucheza nje ya uwanja.

    ReplyDelete
  7. Kuna baadhi ya viongozi wa klabu pinzani wanatumia kila aina ya hila ili Yanga wasichuwe ubingwa. Hili nataka uongozi wa Yanga walijuwe Hilo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa hiyo Hawa viongozi ndo wamewaambia wachezaji wenu wasifunge magoli au wamemwambia yule beki apige mpira na mkono shughulisha ubongo kabla ya kuandika utumbo

      Delete
  8. unaushahidi na hilo la viongozi wa klabu pinzani kuifanyia hila utoo? No research no right to speak! Pambaneni kutafuta ushindi uwanjani na siyo ujanja ujanja.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic