March 4, 2021


 JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao Yanga na wapo tayari kwa ajili ya ushindani kwenye mchezo wao wa ligi wa leo utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Ikiwa imejichimbia nafasi ya 13 na pointi zake 23 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya kwanza na pointi zake kibindoni ni 49.

Timu zote mbili zimecheza jumla ya mechi 21 msimu wa 2020/21 ndani ya ligi. Walipokutana kwenye mzunguko wa kwanza Uwanja wa Mkapa Yanga ilishinda jumla ya mabao 3-0 ambapo ulikuwa ni mchezo wa mwisho kwa Zlatko Krmpotic aliyefutwa kazi mazima.

Kwa sasa kikosi cha Yanga kipo chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze ambaye anakutana ndani ya uwanja na Juma Mgunda wa Coastal Union.

Mgunda amesema:"Tunawahesimu Yanga kabisa kwa kuwa tunajua kwamba wanaongoza ligi, ikiwa mpinzani wako lazima umheshimu hilo lipo wazi.

"Muhimu ndani ya uwanja kucheza fair play hilo la kwanza na pili tupo kwenye ushindani hii ni ligi nasi pia tupo kwenye ushindani muhimu kila mmoja kulitambua hilo.

"Wachezaji wangu wote wapo vizuri kuanzia kwenye mazoezi ya mwisho mpaka morali yao hivyo kikubwa ni kusubiri na kuona. Mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kushuhudia ushindani utakavyokuwa," .


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic