March 4, 2021

 


MSAFARA wa wachezaji 25 wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes umewasilia salama  jijini ,Khartoum, Sudan.

Kikosi kilikwea pipa jana Machi 3 na kilipitia Addis Ababa, Ethiopia usiku wa kuamkia leo kilianza safari kuibukia Sudan ambapo kimeweza kufika salama.

Orodha ya nyota hao ambao ni wachezaji 25 hii hapa:-

Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim, Shomari Kapombe, Joash Onyango, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Mohamed Hussein, Jonas Mkude, Rarry Bwalya, Mzamiru Yassin.

Luis Miquissone, Hassan Dilunga, Ibrahim Ajibu, Clatous Chama, Francis Kahata, Meddie Kagere, John Bocco.

Miraji Athuman, Kope Mugalu, Peter Muduhwa, Tadeo Lwanga, Kenedy Juma na David Kameta. 

Machi 6 kinatarajiwa kuwa na mchezo wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Al Merrikh ambayo ipo nafasi ya nne ikiwa haijaambulia pointi.

Hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa wapinzani wao wakisaka pointi tatu mbele ya Simba ambayo nayo inahitaji pointi hizo.

2 COMMENTS:

  1. Kila la kheri MNYAMA. Mwenyezi Mungu awatangulie katika kila hatua na mmwishowe matokeo chanya yapatikane. Wote tuseme Amina

    ReplyDelete
  2. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Simba Sports Club.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic