MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Yanga, raia wa Burundi, Fiston Abdulazack amesema kuwa suala la sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania wachezaji walifanya uzembe kwa kujisahau baada ya kutangulia kufunga.
Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abed, Machi 7 ambao ulikuwa ni wa mwisho kwa benchi la ufundi lililokuwa likiongozwa na Cedric Kaze nyota huyo alifunga bao mapema.
Nyota huyo amesema kuwa mwalimu aliwaambia siku moja kabla ya mechi na hata siku ya mechi kwamba wamekuwa wakifungwa kwa mipira iliyokufa hivyo wanapaswa waongeze umakini.
Ilikuwa dakika ya 41 alifunga bao la utangulizi na kuwafanya Yanga waamini kwamba wamekamilisha kazi ya kusaka pointi tatu na dakika ya 89 Pius Buswita alifunga bao liliwatoa kwenye reli ya kusepa na pointi tatu.
Nyota huyo ambaye ni ingizo jipya ndani ya Yanga akiwa amesaini dili la miezi sita amesema kuwa wanaopaswa kulaumiwa kwa matokeo hayo ya sare ni wachezaji.
"Naweza kusema kwamba sisi wachezaji tunapaswa kulaumiwa kwa sababu ilikuwa ni furaha tukiamini kwamba tumeshinda ilihali bado tuna kazi ya kufanya kulinda na kuongeza bao jingine.
"Mwisho wa siku kujisahau kwetu kumetuponza licha ya kwamba mwalimu alituambia kwamba makosa yetu yapo kwenye mipira iliyokufa na tukafungwa kwa mipira iliyokufa," amesema.
Kwa sasa Yanga ipo kwenye mchakato wa kumtafuta kocha mpya ambaye atakuja kurithi mikoba ya Kaze ambaye amekiacha kikosi kikiwa nafasi ya kwanza na pointi 50.







ingekuwa sawa kama na yeye ungemuiita yule muuaji wa Yanga Buswita namna vile ambavyo huwa mnaandika ikitokea mchezaji wa timu nyingine akiwafunga Simba mnaandika..
ReplyDeleteJe mwandishi bado hujamuuliza Buswita mtu alitaka kuwafunga Yanga afanyeje? halafu utuandikie Buswita amesema ukitaka kuifunga Yanga fanya hivi
Kutokana na makocha wote hao waliotimuliwa ni Plujin ndie aliekuwa bora kuliko wote ambaye alihakikisha mafanikio mengi kuliko karibu wote waliotangulia, lakini ilipo tokea kidogo tu kufungwa yalisahauliwa yote mema yake na kutimuliwa. Ni lazima tukumbuke kuwa sie kocha tu ndie sababu ya kupata ushindi lakini wa kwanza ni wachezaji wenyewe, ikiwa wachezaji ndio wabovu basi kocha hatoweza kuleta mafanikio, mwalimu mzuri ni lazima apate wanafunzi waziri na huku wakipata maslaha yao. Haiwezekani kuwa karibu mwaka tu kutimuliwa makocha wane na eti wote hawafai.
ReplyDelete