KOCHA mkuu wa kikosi cha klabu ya Simba, raia wa Ufaransa, Didier Gomes amesema kuwa anafurahia kuona safu ya ulinzi ya kikosi chake ikionyesha kuimarika katika siku za hivi karibuni.
Gomes mpaka sasa hajaonja machungu ya kupoteza mchezo ndani ya kikosi cha Simba, ambapo tayari ameiongoza timu hiyo kwenye michezo tisa ya mashindano rasmi, akishinda mara sita na kutoa sare tatu.
Akizungumzia ubora wa kikosi chake Gomes amesema: “Nafurahi kuona kikosi changu kikiwa imeimarika sana katika siku za karibuni kulinganisha na hapo awali, tunaonekana kuwa na ubora mkubwa katika kuzuia kwa kuwa tumefanikiwa kupunguza idadi ya mabao ya kufungwa,"
Simba kesho kutwa Jumanne inatarajiwa kucheza mchezo wao wa nne wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Al Merrikh, utakaopigwa siku ya Jumanne ya wiki ijayo.
Washambuliaji hawazitendei haki nafasi zinazopatikana, kunahitajika straika makini
ReplyDeleteNi kweli unavyosema kuwa mafoward hawatendei haki nafasi wanazopata.Binafsi na ni ukweli japo pengine mashabiki wenzangu hawatapenda kusikia kuwa naona viwango vya Kagere na Bocco vimedrop.
DeleteMajeruhi ya mara kwa mara kwake Bocco inaadhiri sana score board.Spirit ya fighting ya Bocco si kama enzi zake tuanavyomfahamu pengine ya kuwa sasa ni spana mkononi au mwili umeshaanza kuchoka.Kagere ni dhahiri uwezo wake wa kufunga umepungua na pengine anaadhiriwa na mifumo ya makocha au mwili unaanza kukutaa kumtii.Mugalu ni striker mzuri na ananikumbusha enzi za Felix Sunzu wa Simba chini ya kocha Milovan Cirkovic lkn naye Papa Mugalu ni spana mkononi.
Simba tunahitaji striker wa aina na umri kama Prince Dube.
Ulinzi na ongezeko la mzimbabwe Peter Muduhwa liko salama.Viungo wote walioko kwa sasa Simba wako na ubora usio tia mashaka.
Tusubiri mechi zilizo baki ndio tuone ubora wao
ReplyDelete