March 8, 2021


 IMEELEZWA kuwa miongoni mwa makocha ambao wanatajwa kubeba mikoba ya benchi la ufundi ndani ya kikosi cha Yanga kilichokuwa kikinolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ni pamoja na Mecky Maxime.

Kaze na benchi lake la ufundi, jana Machi 7 walifungashiwa virago kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo kwa mujibu wa uongozi.

Timu hiyo mchezo wake wa mwisho kwa mzunguko wa pili kushinda ilikuwa mbele ya Mtibwa Sugar ambapo  ubao Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 1-0 Mtibwa Sugar.

Kwa mujibu wa Yanga benchi la ufundi litatangazwa hivi karibuni kabla ya ligi kuendelea kushika kasi mzunguko wa pili.

Maxime ambaye amefutwa kazi ndani ya Kagera Sugar anatajwa kuwa kwenye mazungumzo na baadhi ya viongozi ili kuweza kumpa kazi hiyo ya kuwanoa vinara hao wa ligi.

Mbali na Maxime pia Kocha Etienne Ndayiragije ambaye alichimbishwa ndani ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jina lake pia linatajwa kuwa miongoni mwa makocha ambao wanaweza kurithi mikoba ya Kaze.


22 COMMENTS:

  1. aje huyo kocha! labda atarudisha desturi ya Saleh Jembe kutuwekea msimamo wa ligi...
    Tulifurahi sana na tulipenda mlipokuwa mnatuwekea mara kwa mara hadi msimamo wa ligi ya wanawake...sasa hivi kimya mnafikia hatua ya kushusha futa habari ya msimamo wa ligi muda mchache baada ya kuwa mmeiandika..

    ReplyDelete
  2. Huyu mrundi atabebeshwa zigo la majanga tu kipindi hiki sio Cha kuwa kocha wa yanga timu ipo na pressure kubwa sana

    ReplyDelete
  3. Ndayiragije aachane na yanga atajishushia heshima ya kazi yake Kama alitaka kufanya hivyo Bora asubiri msimu uanze upya ndio apewe mikoba kwasasa team management haiko sawa ni lawama tu

    ReplyDelete
  4. Naona Yanga sasahivi kama waliofumba macho na huku wakitembea. Inabidi watulie na wajuwe walifanyalo

    ReplyDelete
  5. Afadhali arudishwe babu yetu Hans Van De Pluijm angalau timu ilikuwa inacheza mpira wa kuonekana lakini sio hawa wahamasishaji type ya Julio

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mie ni shabiki mkubwa wa Simba lkn kama mna nia ya kumrudisha Babu Hans Van De Pluijm basi hapo Yanga itakuwa kwenye mikono salama angalau kwa asilimia 80.Nina-heshimu football coaching tactics za Babu Hans.Lakini atakubali kurudi Kidimbwini huku akiwa bado anawadai?

      Delete
  6. Yanga watashangaza sana kama watawachukua makocha waliofukuzwa kwa utendaji mbovu kwenye team walikuwa.watafute kocha Mtaalamu wamkabidhi team.hata Mwambusi hafai.

    ReplyDelete
  7. Mkataba wa Kaze ni miaka miwili, jee kuuvunja mapema si lazima itabidi kulipwa mamilioni wakati ambao Tambwe mwenye kudai milioni arbaini Mpaka leo hii hajalpwa juu ya amri ya fifa alipwe haki zake Auuuuu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwenye mkataba kuna kipengele kinachosema, kwa mfano ufanisi ukiwa chini ya 70% mkataba utavunjwa bila fidia. Mechi 3 za mwisho kapata point 4 kati ya 9

      Delete
    2. Ameondoka utopolo wanaongoza ligi ufanisi umezidi hizo asilimiahalafu hakuna moataba kamaunavyotamka

      Delete
  8. YANGA YAZANZA HARAKATI ZA MAZISHI ...SIKU CHACHE TU..BAKI KUZIKWA

    ReplyDelete
  9. Msenge msola ndio tatzo na sio kocha

    ReplyDelete
  10. Viongozi wanailoga timu icheze vbaya na matokeo mabaya alafu wa ili wamuondoe kocha wakati timu imekosa matokeo wasiomtaka anaondoka

    ReplyDelete
  11. Soka ndio lilivyo tatizo la ushabiki wa juu juu, hamuoni liverpool ilivyokuwa Bora lkn msomi huu inachechemea, tatizo la sisi waTz tunataja matokeo ya haraka na kusahau falsafa ya mpira,
    Yanga na Simba kufukuza Coach ni kitu cha kawaida labda kama mtu ameanza kushabikia mpira mwaka Jana ndio anaweza kushangaa

    ReplyDelete
  12. Simshauri kocha yeyote ajiunge Yanga kwa sasa, ni hatari kwa CV yake

    ReplyDelete
  13. Watakoma mwaka huu wacha waendeleze undumila kuwili wao mwisho wa siku hawataambulia kitu

    ReplyDelete
  14. kocha hana makosa tatizo ni uongozi wa klabu wanachukua maamuzi bila kufikiri kwanza

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic