IMEELEZWA kuwa miongoni mwa makocha ambao wanatajwa kubeba mikoba ya benchi la ufundi ndani ya kikosi cha Yanga kilichokuwa kikinolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ni pamoja na Mecky Maxime.
Kaze na benchi lake la ufundi, jana Machi 7 walifungashiwa virago kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo kwa mujibu wa uongozi.
Timu hiyo mchezo wake wa mwisho kwa mzunguko wa pili kushinda ilikuwa mbele ya Mtibwa Sugar ambapo ubao Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 1-0 Mtibwa Sugar.
Kwa mujibu wa Yanga benchi la ufundi litatangazwa hivi karibuni kabla ya ligi kuendelea kushika kasi mzunguko wa pili.
Maxime ambaye amefutwa kazi ndani ya Kagera Sugar anatajwa kuwa kwenye mazungumzo na baadhi ya viongozi ili kuweza kumpa kazi hiyo ya kuwanoa vinara hao wa ligi.
Mbali na Maxime pia Kocha Etienne Ndayiragije ambaye alichimbishwa ndani ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jina lake pia linatajwa kuwa miongoni mwa makocha ambao wanaweza kurithi mikoba ya Kaze.








aje huyo kocha! labda atarudisha desturi ya Saleh Jembe kutuwekea msimamo wa ligi...
ReplyDeleteTulifurahi sana na tulipenda mlipokuwa mnatuwekea mara kwa mara hadi msimamo wa ligi ya wanawake...sasa hivi kimya mnafikia hatua ya kushusha futa habari ya msimamo wa ligi muda mchache baada ya kuwa mmeiandika..
Saleh jembe ni yanga damu?
ReplyDeleteUlikuwa hujui
DeleteHuyu mrundi atabebeshwa zigo la majanga tu kipindi hiki sio Cha kuwa kocha wa yanga timu ipo na pressure kubwa sana
ReplyDeleteNdayiragije aachane na yanga atajishushia heshima ya kazi yake Kama alitaka kufanya hivyo Bora asubiri msimu uanze upya ndio apewe mikoba kwasasa team management haiko sawa ni lawama tu
ReplyDeleteNaona Yanga sasahivi kama waliofumba macho na huku wakitembea. Inabidi watulie na wajuwe walifanyalo
ReplyDeleteAfadhali arudishwe babu yetu Hans Van De Pluijm angalau timu ilikuwa inacheza mpira wa kuonekana lakini sio hawa wahamasishaji type ya Julio
ReplyDeleteBig up
DeleteKweli
DeleteMie ni shabiki mkubwa wa Simba lkn kama mna nia ya kumrudisha Babu Hans Van De Pluijm basi hapo Yanga itakuwa kwenye mikono salama angalau kwa asilimia 80.Nina-heshimu football coaching tactics za Babu Hans.Lakini atakubali kurudi Kidimbwini huku akiwa bado anawadai?
DeleteYanga watashangaza sana kama watawachukua makocha waliofukuzwa kwa utendaji mbovu kwenye team walikuwa.watafute kocha Mtaalamu wamkabidhi team.hata Mwambusi hafai.
ReplyDeleteMkataba wa Kaze ni miaka miwili, jee kuuvunja mapema si lazima itabidi kulipwa mamilioni wakati ambao Tambwe mwenye kudai milioni arbaini Mpaka leo hii hajalpwa juu ya amri ya fifa alipwe haki zake Auuuuu
ReplyDeleteKwenye mkataba kuna kipengele kinachosema, kwa mfano ufanisi ukiwa chini ya 70% mkataba utavunjwa bila fidia. Mechi 3 za mwisho kapata point 4 kati ya 9
DeleteAmeondoka utopolo wanaongoza ligi ufanisi umezidi hizo asilimiahalafu hakuna moataba kamaunavyotamka
DeleteYANGA YAZANZA HARAKATI ZA MAZISHI ...SIKU CHACHE TU..BAKI KUZIKWA
ReplyDeleteMsenge msola ndio tatzo na sio kocha
ReplyDeleteViongozi wanailoga timu icheze vbaya na matokeo mabaya alafu wa ili wamuondoe kocha wakati timu imekosa matokeo wasiomtaka anaondoka
ReplyDeleteSoka ndio lilivyo tatizo la ushabiki wa juu juu, hamuoni liverpool ilivyokuwa Bora lkn msomi huu inachechemea, tatizo la sisi waTz tunataja matokeo ya haraka na kusahau falsafa ya mpira,
ReplyDeleteYanga na Simba kufukuza Coach ni kitu cha kawaida labda kama mtu ameanza kushabikia mpira mwaka Jana ndio anaweza kushangaa
Simshauri kocha yeyote ajiunge Yanga kwa sasa, ni hatari kwa CV yake
ReplyDeleteWatakoma mwaka huu wacha waendeleze undumila kuwili wao mwisho wa siku hawataambulia kitu
ReplyDeleteUndumila kuwili ganii???
Deletekocha hana makosa tatizo ni uongozi wa klabu wanachukua maamuzi bila kufikiri kwanza
ReplyDelete