March 9, 2021

 


IMEELEZWA kuwa baada ya Cedric Kaze raia wa Burundi kufutwa kazi ndani ya kikosi hicho mikoba yake atakabidhiwa mzawa Juma Mwambusi ambaye alikuwa kocha msaidizi wa timu hiyo.

Mwambusi alijiweka kando ndani ya Yanga kutokana na kile ambacho alieleza kwamba hakuwa kwenye afya bora na alishauriwa  ajitenge na kazi ambazo zitahusisha kelele ama kuzungumza kwa muda mrefu.

Baada ya kutwaa Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar akiwa na Kaze, Mwambusi aliomba kujiweka kando na Mwenyekiti wa Yanga Mshindo Msolla alithibitisha suala hilo.

Hivi karibuni Mwambusi alisema kuwa yupo fiti kiafya baada ya kurejea kwenye ubora wake jambo ambalo linatoa nafasi kwake kurejea kwenye majukumu ya kufundisha.

"Kwa sasa ninaendelea salama na nipo sawa hivyo nina amini kwamba ninaweza kurejea kwenye majukumu yangu hali itakapokuwa sawa kwa asilimia 100," alisema.

Kwa sasa Yanga haina benchi la ufundi baada ya Kaze kufutwa kazi Machi 7 baada ya ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kusoma 1-1 na kufanya timu hiyo kugawana pointi mojamoja na Polisi Tanzania.

Ipo nafasi ya kwanza na ina pointi 50 kibindoni ndani ya Ligi Kuu Bara ambapo ilianza mzunguko wa kwanza ikiwa na Mwambusi pamoja na Kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic ambaye naye alifutwa kazi.

Kesho timu inatarajiwa kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ligi mzunguko wa pili.

1 COMMENTS:

  1. 😍😍😍😍😍😘Allah akutie nguvu pia akuepushe na mahasidi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic