BAADA ya kukamilisha taratibu za kushughulikia matatizo ya kifamilia aliyoyapata hivi karibuni, beki mpya wa klabu ya Yanga, Dickson Job tayari amejiunga na kambi ya kikosi hicho na kuahidi kuuwasha moto.
Job hajaichezea Yanga mchezo wowote tangu kukamilika kwa usajili wake mwezi Januari mwaka huu akitokea ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro, kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo majeraha na matatizo ya kifamilia.
Nyota huyo alitarajiwa kuripoti kambini jana Jumamosi, na kuanza mzoezi ya pamoja na wenzake waliokuwa wakijiandaa na mchezo wa leo, dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa katika dimba la Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Akizungumzia kurejea kwake, Job amesema: “Baada ya kumaliza changamoto za kifamilia ambazo zilinikumba hivi karibuni, nimerejea kuijiunga na kikosi tangu jana Jumamosi kwa ajili ya kujiandaa na michezo iliyo mbele yetu.
“Sijapata nafasi ya kuichezea
Yanga mpaka sasa kutokana na changamoto mbalimbali, lakini naamini kwa kuwa
kila kitu sasa kimekaa sawa, nitajitahidi kuhakikisha najituma kuisaidia kila
nitakapopata nafasi ya kucheza,”
Usiongee sana dogo, subir uanze kucheza ufanye kazi yako.
ReplyDelete