BEKI wa kulia wa kikosi cha klabu ya Simba, Shomari Kapombe ametamba kuwa kikosi cha timu hiyo kimejipanga vizuri kuhakikisha kinafika mbali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
Simba jana ilikuwa na kibarua kigumu cha mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ugenini dhidi ya Al Merrikh ya Sudan, mchezo uliopigwa katika uwanja wa Al-Hilal nchini Sudani na kuisha kwa suluhu.
Simba inaongoza kundi lao baada ya kujikusanyia pointi saba baada ya kucheza michezo mitatu ya awali.
Akizungumzia mipango yao kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya klabu, Kapombe amesema: “Tumekuwa na wakati mzuri msimu huu, ni jambo zuri na la kujivunia kwetu kama timu.
“Kikosi kimekuwa na ushirikiano mkubwa na bila shaka kuendana na plani ambazo tunazo naamini tutafika mbali katika michuano hii kulinganisha na misimu mingine tuliyoshiriki,"
Shida magoli
ReplyDeleteMachache
Pointi ndio muhimu sana
ReplyDeleteFunga weww magoli tuone wacheni upimbi
ReplyDelete