March 7, 2021



JURGEN Kloop, Kocha Mkuu wa Klabu ya Liverpool amesisistiza kuwa ikiwa atafutwa kazi ndani ya timu hiyo kwa sasa kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo haoni mbeba mikoba yake ambaye anaweza kufanya vizuri zaidi yake.

Mwendo ambao anakwenda nao kwa sasa ndani ya Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England unafanishwa na ule wa msimu wa 2014/15 zama zile alipokuwa akikinoa kikosi cha Borussia Dortmund ambacho kinashiriki Bundesliga.

Klopp kwa sasa kikosi chake asilimia kubwa nyota wake wa kikosi cha kwanza wanatibu majeraha ya muda mrefu ambapo huduma ya nyota wake, Virgil van Dijk, Joe Gomes na Joe Matip ambao bado hawajarejea ndani ya uwanja anakosa.

Kocha huyo amesema kwamba wapo watu ambao wanafikiria ameishiwa mbinu na hawezi kufanya vizuri jambo ambalo anaamini yeye ni kwamba hakuna anayeweza kubadili kila kitu hata akiletwa kocha mpya hakuna ambaye anaweza kufikia ubora wake.

"Nadhani kwamba kuna mtu anafikira kwamba anaweza kuja kocha mpya hapa sawa hilo sikatai kwa sababu mimi sina maamuzi. Lakini ipo wazi kabisa kwa kuwa wao wana maamuzi hiyo kwangu sio kesi katika hilo ambalo wataamua.

"Ila ukweli ni kwamba hakuna kocha ambaye anaweza kufanya vizuri, nadhani hakuna ambaye anaweza akafanya vizuri kwa namna ambavyo wanafikiri kwa sasa bado ni lazima kuwa na muda wa kufikiria na kuamua hivyo ni suala la kusubiri.

"Ilikuwa ni kama nilivyokuwa ndani ya Drtmund, hali ilikuwa mbaya ila wachezaji wangu wengi walikuwa ni mejeruhi sikuwa na chaguo wala jambo la kufanya." amesema.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic