Mshauri Mkuu wa masuala ya mabadiliko wa klabu ya Yanga, Senzo Mbatha amewaomba mashabiki wa timu hiyo waendelee kuwasapoti, kwani uongozi unaendelea kupambana kuijenga timu hiyo ili izidi kuwa bora.
Yanga imekuwa na mwenendo wa kusuasua katika michezo yake ya hivi karibuni ambapo Alhamisi iliyopita ilikubali kipigo cha mabao 2-1 katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, hivyo kumaliza mwendo wao wa michezo 21 ya ligi Kuu bila kupoteza.
Licha ya kipigo hicho dhidi ya Coastal, Yanga imeendelea kushikilia usukani wa msimamo wa ligi, na pointi zao 49 walizokusanya baada ya kucheza michezo 22.
Yanga leo inashuka tena uwanjani kujiuliza mbele ya Polisi Tanzania, mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Akizungumzia mwenendo wa klabu hiyo, Senzo amesema: “Tumepoteza mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union, ulikuwa mchezo mgumu kutokana na ukweli kwamba wachezaji wetu walipambana, ili kupata matokeo mazuri lakini hali haikuwa kama ilivyokuwa matarajio yetu.
“Tunajua kuna vitu vingi ambavyo
tunapaswa kuvirekebisha kama timu, na tuna imani benchi la ufundi chini ya
kocha mkuu, Cedric Kaze tutaweza kumaliza mapungufu yaliyopo na kurejea tena
katika hali ya ushindani kama ilivyokuwa awali,’
Nawe mwenyewe ujiangalia maana walikuchukua kwa mihemko tu
ReplyDeleteImeanza kweli kurejea kwenye ubora wake ametoka kufungwa na coastal union Leo katoa suluhu na polisi Tanzania kweli inaonyesha wameanza kutibu majeraha sasa
ReplyDeleteAna wsiwasi huyo na kibaruwa chake kwani baadhi wameshaanza kumunyooshea kidole kwakusema mambo yameanza kwenda kombo baada ya kutua kwake yanga
ReplyDeleteHuyo nae nini alichokifanya. Walimchukuwakwa kishindo nae kuondoka bila ya kwaheri au kukabidhi na alipofika huko ndio mwanzo muanguko wa yanga
ReplyDeleteNyie mikia subirini , Basi hamjakata Kona tutawasikia
ReplyDelete