March 14, 2021


 CEDRIC Kaze, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kama angekuwa bado ndani ya benchi la ufundi angewafunga Simba kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.

Kaze alifutwa kazi Machi 7 baada ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Yanga ilikuwa kwenye mwendo wa kusuasua ndani ya mzunguko wa pili ambapo ilicheza jumla ya mechi sita na kushinda moja, sare nne na ilipoteza mchezo mmoja kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ilikuwa Machi 4.

Kocha huyo amesema kuwa kwenye mchezo wa kwanza ambao alikiongoza kikosi hicho kusaka pointi tatu mbele ya Simba ndani ya Ligi Kuu Bara aliambulia sare ya kufungana bao 1-1 na kugawana pointi moja.

Mchezo wao wa mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa Mei ambapo hatakuwa kwenye benchi la ufundi kwa kuwa ameshafungashiwa virago.

"Ingekuwa bado ningekuwa ndani ya benchi la ufundi la Yanga kuelekea kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba Mei, ninaamini kwamba ningewafunga wapinzani wetu.

"Ninajua kwamba wengi hawawezi kuamini ila huo ni ukweli kwa sababu ninawajua wapinzani wetu vizuri na kwa namna ambavyo walikuwa bora walishindwa kuchukua pointi tatu kwetu.

"Mchezo wangu wa kwanza nilikuwa nina nafasi ya kupata pointi tatu ila aina ya wachezaji wangu walizidiwa mbinu mwishoni lakini kwa namna ambavyo nilikuwa nimewasoma basi mchezo wetu wa pili ningewafunga,"  anasema Cedric Kaze, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga.

9 COMMENTS:

  1. Wakati Simba wanawaza ubingwa wa bara na kufika mbali kimataifa wengine malengo yao ni kuifunga Simba.... Mtasubir sana sana kufanikiwa

    ReplyDelete
  2. Kwake itabaki kuwa historia, maana yeye sio mpinzani wa simba tena kishatemeshwa kibarua. Kama alikuwa anangoja kuwafunga simba ili apate ujiko imekula kwake mazima

    ReplyDelete
  3. Labda ajaye rufaa arudishwe au aombe kazi ihefu au hata kagera

    ReplyDelete
  4. yee anaiwaza simba tuu
    wakati simba inawawaza kina Ahly
    dunia ina viroja mnooo

    ReplyDelete
  5. Ataje timu alizofundisha na mataji aliyochukua kabla ya kuja Yanga . Suala LA Academy ya Barcelona hao wanatafuta vipaji dunia nzima hata Mzumbe academy yetu ina mahusiano na Barcelona kupitia Aspire na huwa scout wao wanakuja siku ya mchujo. Labda angekuwa LA Masia lakini Canada hapana

    ReplyDelete
  6. Lipangala huo ni unafikiwa kiwango cha juu.Mbona maswali haya hukumuuliza alipo kuwa anafundisha Yanga!!

    ReplyDelete
  7. Ameshindwa kuwafunga coastal na polisi tena mechi zenyewe anapata mabao ya kubebwa na ball possession coastal aliongoza ndio aje amfunge Simba hizo ni ndoto zq mchana

    ReplyDelete
  8. Anaweweseka huyo baada ya kuchimbishwa kibarua

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic