KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Kenya ni kutokana na makosa yaliyofanyika kwenye ulinzi.
Stars ikiwa Uwanja wa Nyayo katika mchezo wa kirafiki imepoteza kwa mabao 2-1 jambo ambalo limempa somo Poulsen.
Mabao ya Kenya yalifungwa na Erick Kabaito dakika ya 20 na liliwekwa sawa na Ayoub Lyanga dakika ya 32.
Bao la ushindi la Kenya lilifungwa na Abdalah Hassan dakika ya 59 na kuwafanya Stars wapoteze mchezo wa kwanza na wanatarajia kukutana tena uwanjani Machi 18.
Poulsen amesema kuwa kikosi chake kilifanya makosa mengi kwenye sehemu ya ulinzi jambo lililowafanya wapinzani wao watumie makosa ambayo wameyafanya.
"Nimegundua kwamba tumepoteza kwa kuwa tumefanya makosa mengi upande wa ulinzi, hilo ni somo kwa ajili ya mechi zijazo ambapo tutafanyia kazi makosa hayo.
"Pia wapo wachezaji ambao hawapo ndani ya kikosi watakapojiunga na timu itakuwa rahisi kwetu kuwa na upana wa kikosi zaidi hivyo safari bado inaendelea," .
Blah blah nyingi tuu
ReplyDeleteHakuna jipya kocha komaa tu
ReplyDeleteAmna timu majanga tu twende ivyoivyo ili cku ziende
ReplyDelete