March 15, 2021

 


MZUNGUKO wa pili unaambiwa vita ni kila mahali inazunguka na inaishi kabisa mpaka unajiuliza mara mbilimbili hii ni vita kweli ama mpira maana hakuna burudani tena ngoma imegeuka sasa hakuna amani tena.

Yaani ukisema uwe shabiki huku balaa ni vita ile yenyewe ya maneno tena makali kabisa. Kwa sasa ni rahisi kumsikia shabiki akisema kwamba nitamchapa bakora kiongozi fulani ama nitampiga mwamuzi fulani yaani tafurani kabisa.

Hali hii katika ule ukweli ni mbaya na haipaswi kupewa sapoti hata kidogo kwa kuwa maneno huwa yanaumba na kwa kuwa maneno ambayo yanaumbwa ni ya vita naona hii vita haipaswi kupewa nafasi kabisakabisa.

Nilikuwa ninafuatilia kwenye mechi nyingi za ligi namna matokeo yanavyopatikana. Naona kwamba kuna timu ambazo hazitaki kabisa kupoteza ama kupata sare hii ni ajabu na sijawahi kuona timu ambayo inashinda mechi zote bila kupata sare ama kupoteza.

Weka kando masuala ya kupoteza turudi kwenye vita ambayo inaundwa kwa sasa hakuna amani tena uwanjani kwa mashabiki wala wachezaji hofu inatawala. Kweli hofu inatawala kwa kuwa sasa ni lazima shabiki awe na hofu juu ya usalama wa wachezaji ndani ya uwanja pamoja na matokeo ambayo watayapata.

Hivi unakumbuka lile pira gwaride ambalo lilichezwa pale Uwanja wa Mkapa wakati ubao ukisoma Simba 1-1 Tanzania Prisons? Ilikuwa balaa mwanzo mwisho hakuna amani yaani ukimtazama kocha wa Simba, wachezaji mpaka mashabiki wote hawaelewi nini kitatokea.

Matumizi ya nguvu yalikuwa makubwa huku wachezaji wakitembeza mabuti ndani ya uwanja. Ile iliyomkuta Mzamiru Yassin na kusababisha kadi nyekundu kwa Jumanne Elifadhili mbona ilikuwa cha mtoto, huyo Shomari Kapombe alibanwa mpaka anadondoshwa chini lakini hakuna ambaye anaonekana kujali.

Ukiweka kando mechi hiyo rejea kwenye mchezo wa Polisi Tanzania 1-1 Yanga, hapo unakutana na kadi nyekundu nyingine kwa mkongwe Kelvin Yondani naye hakuweza kuvumilia alikuwa anatembeza mabuti ndani ya uwanja.

Hii hali naona kwa sasa imeanza kukaa kwenye vichwa vya wachezaji wanaamini kwamba mpira ni vita. Mashabiki hawataki kuona vita ila wanahitaji kuona burudani ndani ya uwanja.

Kwani kuna ulazima kwa wachezaji nao kutumia nguvu nyingi muda wote uwanjani ili kupata ushindi?

Nadhani sio mechi hizi mbili ambazo zimekuwa na matumizi makubwa ya nguvu, rejea Prisons walicheza na Azam FC.

Ukiachana na Prisons na Mbeya City nao ni mwendo wa ubabe katika kusaka matokeo hali hii ni mbaya na mwendo unavyokwenda hapa ikiwa wachezaji hawatabadilika tutashudia kadi nyingi nyekundu.

Hakuna faida kwa mchezaji kumchezea faulo mbaya mchezaji mwenzake. Timu kama Simba na Namungo ambazo zinashiriki mashindano ya kimataifa hawa wanapaswa kulindwa kwanza na wachezaji wenzao.

Baada ya wachezaji kuwalinda basi waamuzi nao wana kazi ya kuwalinda. Kwa mfano mchezaji kama Luis Miquissone, Shomari Kapombe, Jonathan Nahimana, Sixtus Sabilo hawa wakiumizwa ndani ya ligi utawaambia nini mashabiki.

Haina maana kwamba wao wanategemewa ila umuhimu kwenye timu na kila mchezaji kwa sasa tayari gari limewaka kuwapa maumivu ni kuzima magari yao ili waanze kujitafuta wakati ujao.

Jambo la msingi kila mchezaji ni kuweka kando vita ya kukamiana bali wacheze mpira huku waamuzi nao wakifuata sheria 17 za mpira. 

Rejea pia mchezo wa Kombe la Shirikisho wakati Yanga ikishinda bao 1-0 dhidi ya Ken Gold, Uwanja wa Uhuru.

Kiungo mshambuliaji Carlos Carlinhos alionekana akimpiga ngumi mchezaji wa Ken Gold na jambo hilo lilimfanya mwamuzi wa kati amuonyeshe kadi nyekundu.

Hii ni mbaya na ni muhimu kila mchezaji akawa mlinzi wa wachezaji wengine ndani ya uwanja.

1 COMMENTS:

  1. Lawama zote kwa waamuzi na TFF. Tembeza red card hata timu nzima ili kuleta discipline. Pia TFF iwafungie wachezaji wanaoonekana kucheza kivurumai mechi kadhaa. Tunalea ujinga atakuja kufa mtu uwanjani kwa kupigwa mateke na hwa wachezaji mahawayani. Wanajidai eti wamekamia, kamia mpira sio kukamia kuparamia wenzako na refa nae natoa macho tuu, pumbafu kabisa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic