March 14, 2021

 


KOCHA wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa mchezo wao wa marudiano na Al Merrikh kuna haja ya kubadili kila kitu ndani ya uwanja ili kuweka mazingira bora ya kuweza kupata pointi tatu.

 

Gomes amesema maandalizi ambayo anayafanya yana utofauti kwani hata wachezaji ambao walitumika kwenye mchezo wa kwanza wanatakiwa kuongezewa nguvu ya wachezaji wengine ambao walikuwa nje ya uwanja kwa kuwa waliona udhaifu wa Al Merrikh kwa uzuri zaidi.


 Gomes amesema, kuna mbinu mbadala ambazo zinatakiwa kutumika ndani ya uwanja kwa sababu wachezaji wa Al Merrikh wana nguvu kubwa na kasi hivyo wachezaji wake watatakiwa kuanza mashambulizi kuanzia nyuma na kwenda mbele huku wakiwa na nidhamu kubwa ya ukabaji.

 

“Huo ni mchezo muhimu sana kwetu kwa sababu ndiyo utarahisisha kazi yetu ya kwenda kucheza kwenye hatua inayofuta, Al Merrikh kila mmoja aliwaona namna ambavyo wanacheza kwa kasi na nguvu kubwa, timu yangu inatakiwa ilitambue hilo.


"Bahati kwamba kila mmoja anatambua umuhimu wa kupata pointi tatu kwenye mchezo huo. Tutaongeza nguvu ya kucheza kuanzia nyuma kwenda mbele na bila shaka tutafanikiwa,” amesema Gomes.

 

Simba walitoka suluhu kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Al Merrikh, na Jumanne ijayo watakutana tena kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa jijini Dar, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.


Mchezo huo utachezwa bila ya uwepo wa mashabiki kutokana na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kutoa zuio hilo.


Kwenye mchezo wao uliopita wa makundi dhidi ya Al Ahly waliweza kushinda bao 1-0 ambalo lilifungwa na Luis Miquissone mashabiki walipata fursa ya kuona mchezo huo na kuipa sapoti timu hiyo ambayo inaongoza kundi A ikiwa na pointi 7.

6 COMMENTS:

  1. Kwa Kuongeza tu Saleh kwa viongozi na wachezaji wa Simba,wanachama na Mashabiki kwa jumla.Simba imezuiliwa kuingiza Mashabiki kwa Mkapa.kwa kuliangalia Suala hili
    juujuu utaona ni utaratibu wa CAF na masuala ya Corona ila kiukweli bila ya kupepesa macho hii ni figisu.Kiukweli warabu wanahaha jinsi gani wanaweza kuisimamisha Simba na kupunguza pengo la point baina yao. Hapa namzungumzia National Alhaly ya Egypt.Mbaya zaidi Boss wa CAF wa sasa ana ukaribu na urafiki wa ndugu zaidi Alahly kuliko wakati wote kutokana na kuwa mdogo wake Mosimane ndie Kocha wa Alahly kufeli kwa Mosimane klabu bingwa Africa hapana Shaka ni kufeli kwa Patrice,mamelodi na south Africa kwa ujumla. Sisi watanzania tunaweza kuchukulia poa kwenye hili suala kwakuwa sisi wenyewe hatupendani na kutakiana mema ila kwa wenzetu ni tofauti kabisa.Kufanya vizuri Mosimane Alahly ni kufanya vizuri kwa makocha wa south Africa na kuaminiwa zaidi,lakini hapa Kuna hatari Alahly kushindwa kutinga robo fainal klabu bingwa Africa Mara hii timu mwenyeji wa makao makuu ya soka barani Africa na hapa ndipo watanzania hasa watu wa Simba wanatakiwa kuwa makini kupita maelezo. Ushauri wangu kwenye hili ni Kama ifuatavyo.Tunajua Simba ni timu yenye viongozi werevu Sana ila tuliona jinsi gani walivyozidiwa mbinu na Tanzania prison. Mechi ya prison Simba haikushindwa uwanjani ila prison walicheza ile mechi nje ya uwanja Kwanza.prison waliingia uwanjani tayari kwa Vita kupita maelezo wakati Simba na viongozi wao waliichukulia mechi ni ya kawaida sana,kosa la Kwanza.kosa la pili Simba imekuwa ikichezewa faulo za hovyo kila zinapokutana na timu za jeshi lakini maamuzi ya marefaree yamekuwa hatarishi kwa wachezaji Kama sikosei hata Boko aliumia kwenye mechi ya prison kule sumbawanga ila viongozi wa Simba wamekuwa wapole mno kukemea hii Hali.
    Kwa mechi ya Almerekh hii mechi ni kuliko fainali kwa Simba na ikiwezekana kushinda kwa magoli mengi kwani vita na Alahly wanamtaji mzuri wa magoli hatujui huko mbele Hali itakuwa vipi.
    Suala jengine viongozi wa Simba wajitahidi na kusimamia kuwaelekeza Mashabiki wao kuwa watulivu na kufuata utaratibu ulioekwa na CAF kwenye mechi hii isije kutokea sababu ya Simba kuazibiwa na kunyanganywa points.
    Suala jengine viongozi wa Simba wawe makini na vipimo vya korona isije ikatokezea sababu ya wachezaji wao wakutumainiwa zaidi wakasimamishwa kucheza.
    Suala jengine Simba wanatakiwa kuwa makini zaidi na Senzo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic