March 15, 2021


IMEELEZWA kuwa Juma Mwambusi, Kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga atakiongoza kikosi hicho kwenye mechi zote ambazo zimebaki ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Mwambusi alirejeshwa kazini mara baada ya Cedric Kaze ambaye alikuwa Kocha Mkuu pamoja na Nizar Khalfan ambaye alikuwa msaidizi wake kufutwa kazi Machi 7 kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni matokeo mabovu.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa sababu za kulifuta benchi la ufundi lililokuwa likiongozwa na Kaze ni matokeo mabaya.

"Ikiwa ni timu inapata matokeo mabaya hapo ni lazima sababu itafutwe na baada ya kutafuta sababu ikaonekana kwamba makosa yapo kwenye benchi la ufundi.

"Hivyo tukakubaliana kwamba ni lazima benchi lifutwe. Kwa sasa tupo kwenye mchakato wa kumsaka kocha mpya ambaye atakuja hivi karibuni ndani ya kikosi chetu.

"Zaidi ya CV 72 zimepokelewa na mchujo unafanyika ili kupata kocha ambaye atakidhi vigezo kabla ya kumtangaza na tunaamini kwamba atakuwa kocha mzuri hivyo mashabiki wasiwe na mashaka," amesema.

Habari zimeeleza kuwa Yanga imekubaliana na Mwambusi ambaye alijiweka kando kwa muda ndani ya kikosi hicho kutokana na matatizo ya kiafya kusimamia kikosi hicho mpaka msimu wa 2020/21 utakapokamilika. 

Kwa sasa Yanga nafasi ya kwanza na ina pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 23 ndani ya Ligi Kuu Bara.

4 COMMENTS:

  1. Hela za kumleta kocha mkuu HAMUNA Nyie uto de Utelembwe de ngederenyani

    ReplyDelete
  2. BREAJING NEWS: Paka wetu wameruhusiwa na CAF kuingia uwanjani.Hii ni kwa mujibu wa barua iliyoka CAF kuja Simba.Barua hiyo ilijibu rufaa ya Simba pamoja na kuruhusu wale paka wetu kuingia uwanjani

    ReplyDelete
  3. Hahahahahaaa paka ndio walioruhusiwa kuingia uwanjani kuna mechi badala ya mashabiki du!

    ReplyDelete
  4. GSM wamesema hawalipii walimu wa riadha . Kutembeza kapu kuna shida ya muda.Kocha huyo huyo atatufaa.Shuka likiwa fupi unakunja miguu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic