WIMBO mkubwa kwa sasa umekuwa ni kuhusu waamuzi kushindwa kwenda na kasi ndani ya uwanja katika mechi ambazo wanachezesha jambo ambao linarudisha nyuma maendeleo ya soka letu.
Ipo wazi kwamba msimu huu ushindani umekuwa
mkubwa huku kila timu ikionekana kupambana kwa hali na mali kusaka ushindi
ndani ya uwanja.
Hesabu kubwa kwa timu zote ni kupata
ushindi na matokeo chanya ila mwisho wa siku kila baada ya dakika 90 kukamilika
wapo ambao wamekuwa wakilalamika kwamba wanashindwa kupata matokeo kutokana na
waamuzi.
Ikiwa kila ambaye anashindwa kupata matokeo
chanya anageukia kwa waamuzi hili sio afya kwa soka letu kwa kuwa pale ambapo
presha inakuwa kubwa inakuwa ngumu kwa timu kuweza kufikia malengo.
Jambo la msingi ambalo ni wito wangu ni
kwamba kila mtu ndani ya uwanja atimize majukumu yake na itafanya haya
malalamiko yaweze kupungua kwa kuwa kila jambo linawezekana.
Kwa timu ambazo matokeo yao yamekuwa ni ya
kusuasua ni muhimu kuongeza nguvu kwenye mzunguko wa pili ili kuweza kupata
matokeo chanya.
Inawezekana kwa kila timu kuweza kuwa
kwenye mabadiliko ndani ya uwanja na kupata matokeo ambayo ni mazuri pale
ambapo wataamua na mwisho wa siku watarejesha tabasamu kwa mashabiki wao.
Mashabiki wanapenda kuona ligi yenye
ushindani inayovutia kuitazama kila siku na sio kila baada ya mechi kuisha mtu
unajutia kwa nini ulipoteza muda wako.
Ikiwa kila siku malalamiko yatakuwa ni kwa
waamuzi hii sio afya kwa kuwa soka letu linapaswa lizidi kupanda chati kutoka
hapa lilipo kwani kila kitu kinawezekana.
Kuanzia kwa mashabiki ambao wamekuwa
wakifuatilia soka kwa ukaribu wameanza kubadili nyimbo za kushangilia ndani ya
uwanja na badala yake wanaimba refa.
Kuhusu hili pia ni muhimu waamuzi wakaongeza
umakini zaidi katika kutimiza majukumu yao kwani imani yangu ni kwamba kila
mmoja anatimiza majukumu yake ila makosa hayawezi kuepukika.
Kwa namna ambavyo mzunguko wa pili
unakwenda kuna vita kubwa kwenye suala la kutwaa ubingwa wa ligi pamoja na zile
ambazo zinapambana kushuka daraja.
Vita hii ni nzuri kwa kuwa inafanya
ushindani unakuwa mkubwa hivyo ili izidi kuwa nzuri zaidi ni lazima kwa waamuzi
nao kuwa makini kwenye maamuzi ambayo wanatoa.
Sheria 17 zifuatwe kwa umakini ili
kupunguza kabisa zile kelele na kuweza kufanya hivyo kutaongeza ushindani zaidi
ndani ya uwanja kwa kuwa kila timu inahitaji ushindi.
Duniani kote hakuna mwalimu ambaye anapenda
kuona timu inapoteza kwa kufungwa ikiwa inasaka pointi hata kwenye mechi za
kirafiki pia kila timu inahitaji kupata ushindi.
Mashabiki nao wana kazi ya kuendelea kuzipa
sapoti timu zao ndani ya uwanja ili kuweza kuongeza hamasa kwani mpira
unahitaji mashabiki. Pia wanapaswa wapunguze presha ndani ya uwanja.
Ipo wazi kwamba mashabiki ni sehemu ya
mafanikio ya timu kuweza kupata matokeo ila ikiwa watakuwa wanazomea muda wote
na kuzipa presha timu zao zitawafanya wachezaji washindwe kutulia.
Ukweli ni kwamba ili timu ifanye vizuri ni
muhimu kila kitu kikawa kwenye mpangilio mzuri. Imani yangu ni kwamba jambo pekee
ambalo linatakiwa ndani ya uwanja ni maandalizi mazuri na kujipanga katika kila
jambo.
Timu zote pamoja na wachezaji ni muhimu
kutambua kwamba ushindani ndani ya ligi unazidi kukua kila iitawapo leo na kila
timu inahitaji ushindi ndani ya uwanja.
Pia ikiwa kila kitu kitakuwa sawa na
maandalizi yatakwenda sawa ndani ya uwanja ni mwanzo wa kupata matokeo chanya
uwanjani.
Jambo la msingi ni kuongeza nguvu kubwa
kwenye maandalizi ambayo ni mwanzo wa kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja.
Ikiwa kila mmoja atapambana kusaka
ushindi ndani ya uwanja itatoa fursa ya zile lawama na kelele kutoka kwa
mashabiki kupungua ama kuisha kabisa.
Kitu pekee ambacho wanahitaji mashabbiki
ndani ya uwanja ni kuona kwamba timu inapata matokeo ndani ya uwanja.
Umuhimu wa kila mechi kuwa ni fainali huku
kila waamuzi watakaopewa mechi kuchezesha kuzidisha umakini upo kila wakati.
Jambo la msingi ni kuona kwamba mzunguko
huu wa pili yale makosa ambayo yalikuwa yanafanyika yanapunguzwa ama kuachwa
kabisa.
Ninaona kwamba mzunguko wa pili utakuwa na
ushindani mkubwa zaidi kuliko ule wa kwanza kwa kuwa hapa ni mwisho wa hesabu
kwa timu zote ndani ya ligi.
Ikiwa timu itashindwa kupata matokeo chanya
wakati huu itakuwa ngumu kuweza kufikia malengo ambayo wamejiwekea.
Kila kitu kinawezekana ikiwa kutakuwa na
maandalizi mazuri kwa kuwa kila kitu kwenye mpira kinahitaji maandalizi na
utekelezaji kwa wakati.
0 COMMENTS:
Post a Comment