March 14, 2021


 BAADA ya kupoteza mchezo wa kwanza hatua ya makundi katika Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Raja Casablanca, Kocha Mkuu wa Namungo, Hemed Morocco, amefunguka kuwa kwa sasa wamejikita na maandalizi kuelekea mchezo ujao dhidi ya Pyramids FC unaotarajiwa kupigwa Machi 17, mwaka huu.

Juzi Ijumaa, Namungo ilirejea Tanzania ikitokea Morocco ilipoenda kucheza na Raja Casablanca na kufungwa bao 1-0.


Kesho Jumatatu, kikosi hicho kinatarajia kuingia kambini kujiandaa na mechi dhidi ya Pyramids FC itakayochezwa Dar.


Akizungumza na Spoti Xtra, Morocco amesema: “Tumepoteza mchezo wetu wa kwanza lakini hilo halitukatishi tamaa, tunajipanga kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Pyramids, tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini tutafanya maandalizi ya kutosha ili tuweze kupata matokeo mazuri.

 

“Tutayafanyia maboresho makosa ambayo yalijitokeza kwenye mchezo wetu wa kwanza ambapo tulifanya makosa mengi kwenye eneo la ulinzi jambo lililopelekea tukaruhusu bao la mkwaju wa penalti.”


Namungo inashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza na imefanikiwa kutinga hatua ya makundi.

2 COMMENTS:

  1. Namungo Haina kikosi competitive wanachojaribu kuboresha Ni jinsi ya kuzuia tu na sio kushambulia hivyo naona mwisho wao ni ktk hatua hii ya makundi hawataweza kutoboa quarter final

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic