March 9, 2021

 


KLABU ya soka ya Yanga imemtangaza aliyekuwa kocha wao msaidizi Juma Mwambuzi kuwa kaimu kocha wa Yanga akichukua nafasi ilioachwa na kocha Cedric Kaze.

Yanga juzi Jumapili ilifikia maamuzi ya kuvunja benchi la ufundi la timu hiyo lililokuwa likiongozwa na kocha Cedric Kaze, kutokana na mwenendo mbaya wa timu, ambapo kati ya michezo sita iliyopita ya Ligi Kuu wamefanikiwa kushinda mchezo mmoja pekee.

Mpaka anaonyeshwa mlango wa kutokea juzi usiku, Kaze alikuwa ameiongoza Yanga kwenye jumla ya michezo 25, akishinda michezo 16, amefungwa michezo miwili na kutoa sare mechi saba.

Akizungumzia maamuzi hayo Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dkt. Mshindo Msolla amesema: “Tunategemea mwalimu Mwambusi ataichukua timu wakati tunatafuta mwalimu mkuu.

"Bahati nzuri yeye aliondoka vizuri, amepata matibabu klabu imemsaidia kwenye matibabu yake amepata nafuu. Hana ugeni wa timu tulikuwa nae kwenye Mapinduzi Cup kwa hiyo kurudi kwake sio jambo geni.

“Mwalimu mwingine tutaendelea na taratibu nyingine za kawaida, makocha watatuma CV zao zitakwenda kamati ya ufundi watazipitia na kuona yupi anafaa kwenye klabu yetu kwa sasa.”



5 COMMENTS:

  1. Huyu ndo atafukuzwa mapema sana

    ReplyDelete
  2. hivi si ni yule alikuwa Mbeya City na inaboronga?
    Hata hivyo Yanga hupenda janja janja hapo wanamtumia wakati wakitafuta kocha...baadaye wanamtema au kumshusha awe msaidizi

    ReplyDelete
  3. Utopolooo wanataka mtoto azaliwe leo aanze kukimbia kitu ambacho haliwezekani, kaeni jengeni team

    ReplyDelete
  4. Kuelewa ni kazini sana mwambusi amekaimu na hajatangazwa kuwa kocha mkuu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic